Kipaumbele namba moja kwa mwanaume ni kazi yake, sio mahusiano na mapenzi

The redemeer

JF-Expert Member
Jan 28, 2025
2,438
4,447
Mwanaume ambaye ameacha kazi zake kwa ajili ya kujali mahusiano/mwenza wako huwa anakwenda kupoteza vitu viwili kwa pamoja kwanza anakwenda kumpoteza huyo Mwanamke wake ,kisha anapoteza kazi/ndoto yake.Hivyo maumivu makali sana yanakuwa mara mbili.

Unaweza kupata mshtuko lakini huu ni ukweli mchungu kwamba kipaumbele namba moja kwa mwanaume yeyote Rijali huwa ni kazi yake sio Mwanamke/mahusiano yake.

Kwanini mwanaume kipaumbele chake namba moja ni kazi yake badala ya mahusiano?
Jibu lake lipo ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI sura ya pili leo tuangalie muhtasari wake.

Mwanaume yeyote ambaye ameoa au kutoa barua ya posa anajua kwamba kitu ambacho ukweni huwa wanazingatia sana sio uchamungu,au uaminifu,upole, ustaarabu, unyenyekevu ambao mwanaume anakuwa nao bali wanauliza unajishughulisha na kazi gani kwanza kabla ya kitu chochote.

Kwanini kazi inatangulia badala ya uchamungu, ustaarabu, unyenyekevu,huruma na upole ?
jibu lake ni kwamba vitu kama upole , ustaarabu, unyenyekevu, huruma, uaminifu ni vitu ambavyo mtu anaweza kuwa navyo kisha kesho anabadilka tabia anakuwa tofauti lakini kazi mtu akiwa nayo wanajua unafuu wa maisha umepatikana kisha mwanaume anapopoteza kazi yake mapenzi yanakufa papohapo na utaratibu wa talaka unaanza .

Ni wanawake wachache sana huwa wanakubali kudumu na mwanaume ambaye hana kazi yoyote.Katika wanawake 10 ambao wanakuwa wameolewa 9 huondoka baada ya mwanaume kupoteza kazi au pale ambapo mwanaume anashindwa kuhudumia familia ipasavyo.Vilevile hata hao ambao huwa wanabaki na kuvumilia shida wengi huanza kuonyesha dharau waziwazi,kiburi, majivuno, jeuri wengi huanza kumfanyia udhalilishaji mwanaume kwa makusudi, wengine hufikia hatua anaingiza mabwana nyumbani kwake kwaa makusudi kwa sababu anajua mwanaume hana kazi yoyote hivyo hana sauti.

Ni vigumu sana kwa mwanaume ambaye ni mstaarabu sana, mwaminifu,mpole, mwenye huruma lakini hana kazi yoyote ya kumtunza Mwanamke akaheshimiwa.

Hivyo basi HESHIMA ya mwanaume ipo kwenye kazi yake sio ustaarabu, unyenyekevu, huruma, uaminifu, baina,kujali n.k

Tuangalie mifano michache.
Kwa mfano ukiwa mwanaume ambaye umeishia darasa la saba lakini unamsomesha binti mpaka chuo kikuu kisha upo na matarajio kwamba baada ya binti huyo kumaliza masomo chuo kikuu aje kuwa mwenza wako, uhalisia ni kwamba baada ya binti huyo kumaliza masomo chuo kikuu atakuona wewe sio mwanaume wa HADHI yake kwa sababu tayari anakuwa na mafanikio makubwa zaidi yako hivyo ile HESHIMA yako kwake inatoweka.

Sababu ya heshima yake kutoweka ghafla ni kwamba amekuwa na mafanikio makubwa zaidi yako lakini kipindi alikuwa hajasoma alikuona ni mwanaume wa HADHI yake kwa sababu alikuwa hana kazi yoyote.

Mfano mwengine mwanaume ambaye amekuta Mwanamke hana kazi yoyote wala hana biashara yoyote lakini mwanaume aliamua kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea, kumsomesha, kuwasomesha watoto ambao ametelekezwa nao,kuwasadia ndugu wa binti, kuwajengea wazazi wa binti baada ya mwanaume kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea, kumsomesha, kumchukulia mkopo,kumuandika majina yake kwenye mali za mwanaume ambazo Mwanamke husika hajachangia hata senti tano Mwanamke huyohuyo hutafuta kisingizio cha kuibua ugomvi kisha mahusiano yanavunjika ghafla.
Kwanini inakuwa hivyo ?
ni kwa sababu mwanaume anakuwa amefanya uwekezaji mkubwa sana kubadilisha maisha ya mwanamke wake kuliko kuboresha maisha yake yeye mwenyewe.
Hii maana yake ni rahisi Mwanamke kutulia na mwanaume kama amezaa na mwanaume husika kwa sababu kulea mtoto bila baba huwa changamoto.Kwa maana Mwanamke anapolea mtoto yeye mwenyewe (Single mother parenting) maana yake anakuwa anafanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwanaume wake kwani mtoto akiwa mkubwa atarudi kwa baba yake.

Inapotokea Mwanamke amelea mtoto yeye mwenyewe (Single mother parenting)bila MSAADA wa baba wa mtoto , husababisha Mwanamke anakuwa na hasira kupitiliza,chuki, kinyongo, wivu, kisirani, gubu dhidi ya baba mzazi wa mtoto wake hali ambayo husababisha anamjaza maneno mabaya sana mtoto wake kuhusu ubaya wa baba yake.Ni kwa sababu kulea mtoto ni uwekezaji ndio maana Mwanamke ambaye amezaa huwa rahisi kurudiana na baba wa mtoto wake kwa sababu ya uwekezaji.

Kwanini mwanaume kipaumbele chake namba moja ni kazi yake sio mahusiano?
ni kwaa sababu mapenzi hayatabiriki na vilevile Mwanamke haeleweki anataka nini kwa maana unaweza kumpa Mwanamke kila kitu ili uweze kudumu naye ghafla anaondoka kwenda kwa mwanaume mwengine bila sababu zozote za msingi.

Kazi ni rahisi kutabiri nini kinaweza kutokea siku za karibuni lakini Mwanamke hatabiriki.Kwa kawaida mwanamke anaweza kumpenda sana mwanaume leo lakini kesho asubuhi akiamka anakuwa anamchukia sana mwanaume bila sababu zozote za msingi hii maana yake kwa mwanaume ambaye kipaumbele chake ni mahusiano hujikuta anavurugwa kiakili lakini kwa mwanaume ambaye kipaumbele chake namba moja ni kazi hawezi kuvurugika kiakili kwa sababu anajua Mwanamke hatabiriki kwake anaishi naye kwa akili badala ya hisia.

Hauwezi kuishi na Mwanamke kwa akili kama Mwanamke atakuwa kipaumbele chako namba moja kwa sababu ndani ya muda mfupi hisia za Mwanamke zikibadilika anafanya maamuzi yoyote ikiwemo kuvunja mahusiano ghafla bila sababu zozote za msingi.

Wanaume ambao walifanya uwekezaji mkubwa sana ili kudumisha mahusiano hivi sasa wanalia na wengine wameishia kuwachukia wanawake mpaka maisha yao yote wanajikuta hawana hamu na Mwanamke.

Mwanamke akijua anapendwa sana huanza kuonyesha vituko kama vile kurudi nyumbani kwao mara kwa mara ili kupima upendo ambao mwanaume yupo nao kwake,

Mwanamke akijua anapendwa sana huanza kununa, kutishia muachane,kususa,kufanya vituko vya mara kwa mara,anaweza kuondoka nyumbani bila kuaga kisha anarudi saa 8 za usiku na endapo utauliza kuhusu wapi alikuwa anaporomosha matusi ya nguoni kwa kudai Mwanaume wake amezidi wivu,amezidi kumfuatilia,amezidi kumchunga.

Mwanamke anaweza kuingiza wanaume chumbani kwake anapolala na mume wake bila kujali jasho ambalo mwanaume wake amewekeza ikiwemo kumlisha,kumvisha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea, kumsomesha, kuwasomesha wadogo zake, kujenga nyumbani kwao binti hii ni kwa sababu mwanamke anaishi na kufanya maamuzi kwa hisia zake sio kwa kutumia mantiki (logic).

Mwanamke hatabiriki kwa sababu anaishi kuendeshwa na hisia sio akili (logic).Kwa sababu mwanamke huongea na kufanya vitu kutegemea na hisia zake ni wazi kwamba muda ambao hisia zake zinapobadilika hata tabia yake inabadilika bila kujali umefanya uwekezaji mkubwa sana kwake.

Mwanaume ambaye anajua kwamba Mwanamke hatabiriki hutumia muda mrefu sana kufikiria kuhusu kazi yake,malengo yake na amani ya moyo wake kisha Mwanamke wake akionyesha ushirikiano wanaishi kwa amani na pale ambapo Mwanamke wake haonyeshi ushirikiano wowote anamuacha huru.

Kuishi na Mwanamke kunahitaji akili zaidi kuliko hisia.Ukiwa na hisia kali sana kwa Mwanamke unakwenda kuwachukia wanawake wote ulimwenguni.

Ishi na Mwanamke kwa akili sio hisia kwa sababu hisia za Mwanamke huwa hazitabiriki hivyo upendo wa Mwanamke hautabiriki vilevile.

Ndiyo maana wanaume ambao wamefanya mahusiano kuwa kipaumbele kuliko kazi zao hivi sasa wanalia na kusaga meno.

Mwanamke hatakiwi kuwa kipaumbele namba moja kwa mwanaume bali awe sehemu ya kufanikisha malengo ya familia.Akiwa kipaumbele namba moja anakuvuruga akili pale ambapo hisia zake zinapobadilika.

Kadiri mwanaume anavyomfanya Mwanamke kuwa kipaumbele namba moja ndivyo mwanaume huwa anavurugwa kiakili.

Kuvurugika kiakili kunakuja kwa sababu ya mabadiliko ya hisia kwa Mwanamke
 
Mwanaume yeyeto anaeweka kipaumbele kwenye mahusiano ni lazima ale za uso.
Ndo hao wanaojiua/ au kuua wenzao
 
Hakuna maumivu kuliko ya kutairiwa kuliko maumivu ya mwanaume kuwa kipindi zero, kweli nguvu ya mwanaume ni pesa
 
Apandacho mtu ndo atavuna ukimtesa mme wako kisa Hana kitu siku akipata lazima atakuacha tu hii ni kanuni.
Na mke wako akikupenda hata ukiwa hauna kitu na ukapata ukamuacha utoboi.
Ukiona mwanaume anaendelea kutoboa na mke mwingine tambua aliyekuwa nae mwanzo ndio kimeo.
Wanaume masikini wanateseka sana kwenye ndoa sema tu hawana jukwaa
 
Mfano mwanamke anakuporomoshea matusi mbele ya watu watoto bila aibu kisa una kitu anakuunganisha wewe na ukoo wako wako,anakudharau huna kitu,anakuletea hadi wanaume plus kutukanwa na madharau kibao kisa umedrop,hivi takataka kama hii siku umejipata unakosa gani kwa Mungu ukila kona baada ya kujipata si unavuta chuma ingine kama mzee wa kawe ikuponye makovu ya kudhalilisha kisha umasikini
Halafu ukivuta chuma ingine mke na jamii haichelewi kusema " wanaume sio watu yaani mke wake kamvumilia ehee wakati wa tabu Leo kapata kamuacha" ujui huyo mwanaume ana makovu gani,hakuna mwanamme anaweza muacha mke wa tabu nae zaidi anaweza kuwa na michepuko lkn heshima ipo kwa mke.
Upandacho mtu utavuna
 
Saikoloji ya wanawake wengi wanaamini ukifulia basi milele ndo umefika mwisho wanashindwa kuelewa saikolojia ya nyota ni mzunguko Pana kipindi inapita kwenye Giza kipindi inapita kwenye nuru hii uwapata tabu ukiwa down ukimbikia ukirudi juu wanatamani kurudisha nyuma historia kumbe ilikuwa ni kipimo tu cha kumjua je mwenza wako atabadilika kulingana na Hali?
 
Back
Top Bottom