Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,013
- 2,816
⚠️😳 Kiongozi wa kanisa Katoliki adakwa na vyombo vya usalama Marekani na kuvuliwa wadhifa huo kwa kuishi maisha ya kifahari kwa kufanya utapeli wa zaidi ya shilingi bilioni 1.7 ($650k) ambazo ni michango ya wahisani na waumini kwa ajili ya kusaidia wagonjwa/wahanga wa vita nchini Lebanon
Rev.Powel Bielicki(Father Paul) mwenye miaka 48, alikuwa anadanganya wahisani na waumini kuwa ana clinics nchini Lebanon kwa ajili ya kusaidia wagonjwa katika maeneo yaliyoathiriwa hasa kwa vita, hivyo alikuwa anadai anahitaji michango ya vifaa tiba, ambulances na mengineyo na akishapewa pesa anajifanya kanunua vifaa kumbe pesa anazitumia katika kula bata
Baada ya fununu za utapeli kisha vyombo vya usalama kuanza kumchunguza imebainika hana hata hizo kliniki za afya huko Lebanon
Vyombo vya usalama vimegundua pesa hizo amezitumia kula bata ikiwemo misosi ya gharama katika migahawa ya kifahari, kusafiri maeneo kadhaa, kulipia gym za kihahari na kufanya sajari ya urembo kuukarabati mwili wake azidi kuwa na muonekano wa kuvutia
Kiongozi huyo wa Kikatoliki Marekani mwenye asili ya Poland, alisimikwa mwaka 2001 kwa mujibu wa kanisa
Mawasiliano yake yakiwemo ya emails yamedakwa na vyombo vya usalama akiwahadaa watu kwa maneno matamu watoe pesa za michango katika njia zake za kutapeli
Katika kutapeli watu kuna wakati alikuwa anajifanya yeye ni daktari wa mambo ya upasuaji na kuna wakati alikuwa anajifanya yeye ni mtafiti anayefanya kazi na umoja wa mataifa, pia amebadili majina kisheria kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya usalama
Kwasasa sheria inasubiriwa kuchukua mkondo wake kuhusu mchungaji huyo