Aliyewahi kuwa kiongozi wa Chadema. Nani huyo? Gazeti la Mwananchi.
=========================
Mratibu wa uhamasishaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Twaha Mwaipaya-- ambaye aliachiwa pamoja na Nusrat, anasimulia jinsi walivyotolewa gerezani saa 1 jioni.
Nusrat, Mwaipaya na wenzao walikuwa gereza la Isanga Dodoma wakishtakiwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali, kudhihaki wimbo wa Taifa, kujaribu kuvujisha siri za halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kutoa lugha za kuudhi.
Mwaipaya alisema baada ya kutoka gerezani walifanya mawasiliano na Aisha Madoga ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo wa Mkoa Dodoma ili kumjulisha kuwa wapo huru.
“Tulisubiri muda wa dakika 20. Mtu wa kwanza kuja alikuwa (jina limehifadhiwa) aliyewahi kuwa kiongozi wa Chadema, akitokea ndani ya lango la gereza,” alisema.
“Mimi na wezangu tulishangaa sana kumuona kiongozi huyo na tulimuuliza kumbe hakuwa mbali? Akajibu alikuwa na fununu kuwa tutaachiwa, lakini hakumwambia mtu yeyote ndiyo maana ‘nipo hapa’.”
Mwaipaya alisema kiongozi huyo aliwachukua na kuwapeleka hoteli iliyopo eneo la Kito kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na baadaye Madoga aliwasili.
Alisema baadaye Hanje aliomba kuondoka na mwenyekiti huyo Bavicha mkoa wa Dodoma ili akapumizike.
“Hatukuwa na wasiwasi kwa sababu wote ni wanawake. Hatukuona haja kumzuia, lakini niliagiza Bavicha jimbo la Dodoma kufanya jitihada za kuhakikisha usalama wa Hanje. Walikwenda hadi nyumbani kwa Madogo. Walivyofika Hanje aliomba akampumzike hotelini kutokana na hali ya taharuki aliyokuwa nayo.
“Akapelekwa hotelini na kuhifadhiwa hapo pamoja na kuwekewa ulinzi wa siri na Bavicha. Kesho yake nilimpigia simu Hanje kupitia kwa Madoga, lakini niliambiwa ameshatoka hotelini na hajulikani alikoelekea,” alisema Mwaipaya.
“Tulianza kumtafuta, lakini maelezo tuliyopata Hanje alichukuliwa saa 3:00 asubuhi na kiongozi aliyekuja gerezani akishirikiana na mbunge wa zamani wa viti maalum Dodoma, walioondoka naye, tulijibiwa hawapo na Hanje.”
Alisema jambo hilo lilizua taharuki kwa Chadema lakini baadaye taarifa zikianza kusambaa kuwa wanachama 19 wangeapa kuwa wabunge wa viti maalum, jambo lililoishtua Bavicha.