Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 88
- 62
Maradhi yatokanayo na uoga hutuzalishia ujinga wa fikra.
Ndugu zangu wanaccm na watanzania kwa ujumla ,ninamshukuru kwa baraka zake za kutuwezesha kuiona siku ya leo.
Kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo mwanzo wa maarifa. Nakumbuka mwaka 2019 katika mashindano ya Qur aan Dar es salaam
Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli alisema, ninamnukuu "kumcha Mungu kuna baraka zake." Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 01/02/2021 katika siku ya sheria na miaka 100 ya mahakama kuu,Professor brahim Hamisi Juma alianza kwa kumuomba mungu, alisema ninamnukuu,
"Awali ya yote napenda kuchukuwa nafasi ya kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu mwenye wingi wa fadhila kutuwezesha kukutana kwa mara ya kwanza kabisa katika makao ya nchi yetu dodoma."
Wanaccm na Watanzania wenzangu huu ni uthibitisho ya kwamba tukiamuwa kumtanguliza mungu kwa kila jambo letu ni wazi tutafanikiwa sana .
Basi tuendelee kumuomba Mungu ili atuzidishie ujasiri wa kuacha uoga wa kijinga
tujiamini na kusimamia ukweli bila ya kumuonea mtu bali kwa kujisomea na kufuata maandiko yetu tuliyokubaliana na kuyalinda huu ndiyo utu.
Nakumbuka tarehe 04 09/ 2018 Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa Ukerewe alisema, ninamnukuu,
"Nataka mahali tunapokosea tujisahihishe na mahali tunapopaweza tujipongeze,nataka Tanzania na Watanzania wa namna hiyo." Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma kitabu cha tujisahihishe uk 18 Mwalimu Nyerere anatuelezea, "Mungu ametupa akili ili tuweze kuzitumia kwa manufaa yetu na jumuiya."
Wanaccm na Watanzania wenzangu, suala la kurekebishana sio jepesi , lina chuki na hasama ndani yake
lakini ni lazima tujitoe muhanga ikibidi kufa ni sawa tu ilimradi hatumuonei mtu bali tunasimamia haki na usawa.
Tujiulize kwani wale wote wanaokufa mahospitalini ni wanasiasa? tuache uoga. Tukisoma maandiko Matakatifu ya Biblia wakorintho 10: 3-5
Maandiko Matakatifu yanasema," maana ingawa twaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili." "Maana silaha za vita vyetu si mwili, bali zina uwezo katika mungu hata kuangusha ngome. Tukiangusha mawazo na kila kilichoinuka juu ya elimu ya mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii kristo." Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma kitabu cha tujisahihishe ukurasa 03 Mwalimu Nyerere anatuambia,
Ninamnukuu, " wengine huweza kumuona mwenzao anafanya kosa badala ya kumwambia pale pale kijamaa watanyamaza kimya, lakini watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri mateto hayo si ya kumsaidia, ni ya kumdhuru, hii ni aina moja ya fitna."
Kila Mtanzania anao wajibu wa kuzilinda , kuzitetea na kuchukuwa hatua dhidi ya uvunjifu na usiginwaji wa sheria zetu kuu.
Haya hayatafanyika endapo tutaendekeza maradhi ya ugonjwa wa uoga ugonjwa huu ni hatari kuliko hata. covid 19 kwani unaziumiza hata familia zetu pasipo na sababu za msingi.
Niliwahi kusoma kitabu cha the Magic of Thinking Big. Mwandishi David J Schwartz PH D.
aliwahi kuandika,
"truly, fear is a powerful force. in one way or another fear prevents people from getting what they want from life."
fear of all kinds and size is a form of psychological infection, we can cure a mental infection the same way we cure a body infection with specific proven treatments.
Rais wetu anaiheshimu katiba na Sheria za nchi na aliapa kuzilinda kwanini huku chini watu wanazisigina kisha ni hao hao wanazilaumu Mahakama, DPP, Polisi, TAKUKURU nk.
Tuanze sasa kujilaumu wenyewe wale wote wavunjifu wa sheria kabla ya kuwalaumu wengine kwa makosa yetu ya maksudi kisha ni sisi sisi tunatumia kauli za ukali na tunajitanua , tunavimba makwapa kuwaonea wanyonge kwa vikanuni tunavyoviona vinafaa kuwaonea maskini huku tukiwalinda wakubwa wakubwa hata kama kuna ushahidi ya kwamba wamepora wake za wanyonge na kuwazalisha na mambo mengine mengi ya hovyo.
kwani sisi ni akina nani na wao ni akina nani hadi wavunje katiba zetu waziwazi.
wanajitajirisha tukiwashuhudia huku tukizidi kuwa makapuku ila kwa sababu ya uoga , kujipendekeza, na kujikombakomba na kulamba lamba visigino vyao tumekuwa wakimya.
Ni heri kufa nikisimamia ukweli kuliko kufanywa kikaragosi, kibaraka au kijibwa cha watu fulani kwani baba wa taifa yapo maandiko aliyaacha ametukataza tabia hizo na akatuhusia kuusimamia ukweli na kuacha uoga..
turudi kwenye mstari wote tufuate siasa za ukweli za ujamaa.
Ujamaa sio wachache kujilimbikizia mali huku walio wengi wakitaabika huo ni ubepari tubadilike wenye tabia hizo jamii imeamka inaona wachache wanavyofurahia wakila bata kwenye mahoteli makubwa huku walio wengi wakipambana japo kupata buku jero ya kula kwa mama ntile kwa ugumu mno.
Nawaonya wenye tabia za shibe kuwaonea wanyonge waache. yapo mambo mengi ya kuingiza vipato tukisaidiana.
Sio lazima wanaccm tutesane kwa makosa yaliyofanywa na wachache na yanayoendelea hadi sasa ya kupuuza na kudharau matakwa ya katiba ya ccm kuhusu taratibu za kuwaingiza wanachama ndani ya ccm.
Tukisoma kitabu cha tujisahihishe ukurasa 04 - 05 Mwalimu Nyerere anatukumbusha,
"ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki, kwake watu wote ni sawa.Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama utapuuzwa, ukiona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nukilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikilipiga teke basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. kweli haupendi kupuuzwa puuzwa." Mwisho wa kunukuu
Wanaccm na Watanzania wenzangu kufanikiwa kimaisha ni kuwekeza kwa watu kwa kuwasaidia na kuwainua kama anavyofanya rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Na tuliyobaki tufanye hivyo , tuige matendo mema tuache ubinafsi na roho mbaya kwani matendo ya hovyo ni matendo ya watu wasio fanikiwa kimaisha wa hovyo kabisa hata kama wana mifedha na mali kedekede.
Niliwahi kusoma kitabu cha the Magic of Thinking Big ukurasa 21
Mwandishi David J Schwartz PH D aliwahi kuandika, "unsuccessful people suffer a mind - deadening thought desease. we call this desease exusitis." Mwisho wa kunukuu
Tuache sababu za visingizio tuzaliwe upya kwenye mioyo yetu tuwe na upendo wa kweli tuwasaidie wenzetu wainuke kimaisha . Tusilolipenda tusiwafanyie wengine. tuache tabia za kinafiki za kujiona bora kuliko makapuku walio wengi wanaotaabika.
Tukisoma kitabu cha the Magic of Thinking Big ukurasa 07
Mwandishi David J Schwartz PHD anasema,"nobody enjoys crawling, living in mediocrity. no one likes feeling second class and feeling forced to go that way."Mwisho wa kunukuu
Watanzania wenzangu , kama tunavyohamasisha wanetu kusoma , ni vivyo hivyo na sisi tujisomee tuwe na uelewa ili tuweze kusimama na kujenga hoja zenye mashiko . Tusome ilani ya ccm 2020 ukurasa 128 - 130 kifungu cha 80 na kuendelea.
tusome kitabu cha kanuni za jumuiya ya umoja wa wazazi toleo 2017 ukurasa 01 kifungu cha 02 Tuache kubembelezana tuamue kujisomea ili tukuze uelewa utakaopelekea sisi kwa sisi kutendeana haki na usawa.
tusome katika ya ccm ili tuelewe haki na wajibu wa mwanaccm kujielimisha ili kuuondoa ujinga unaotuzalushia uoga kwa visingizio vya heshima.
Nakumbuka February 2021 Rais wetu mpendwa dkt john pombe joseph magufuli
akizindua kiwanda cha kukoboa mpunga alisema,
ninamnukuu," Tumebembelezana mno kwa kuogopana sura." Mwisho wa kunukuu.
Tupendane Nakumbuka February 2021 Katika maadhimisho ya miaka 44 ya ccm
mzee joseph butiku alisema, ninamnukuu, "nilichotaka kusisitiza kwamba mwl (nyerere) niseme na karume vile vile.
Mwalimu yeye ndiye alikuwa na imani kubwa kabisa na binadamu wenzake, kwa hiyo alitutengenezea hapa itikadi ya ujamaa ina maanisha unaamini katika mambo mawili tu.
la kwanza unaamini ya kwamba binadamu unayemuona karibu yako ni sawa na wewe katika utu wenu. hilo Mwalimu Nyerere hakuwa na mzaha nalo , na ndilo aliloliacha kwenye chama cha mapinduzi. Itikadi ya ujamaa ni kwamba sisi wote ni sawa katika utu wetu. la pili sisi wote tunastahili haki , haki sawa kwa wote.
mwisho wa kunukuu
Watanzania wenzangu najitolea kuwaelimisha kadri ninachojaaliwa kukielewa kwa uelewa wangu kizingatieni.
nia yangu ni kurekebishana ili tuache uoga kwenye mambo ya msingi. Haiwezekani sisi CCM tumeaminiwa na Watanzania wenzetu kuongoza nchi na tukawaahidi tutawaondolea umaskini.
Mwishowe ni sisi sisi tulio wengi tumeendelea kuwa omba omba. ni lazima tufikiri nje ya box ,
kama watu wanavunja katiba ( sheria mama kubebana) iweje tukazanie kanuni kisa tu zinambana mnyonge kwa makosa ya wakubwa wachache waliyokosa ya kuisigina katiba kwa kupuuza utaratibu wa uingizaji Wanachama.
Tuwasaidie wenzetu walio wengi , wanaccm wana maisha magumu sehemu nyingi. Nakumbuka june 2016
Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli akiwaapisha wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa alisema,
Ninamnukuu,"ukifanya kitu kizuri kwa dhamira yako iliyo njema kitazaa matunda mazuri."ukifanya kitu kwa unafiki hakitafanikiwa." Watanzania wanateseka sana , ni mengi yanayofanyika ya ajabu, mengi." Mwisho wa kunukuu.
Wanaccm wenzangu na watanzania kwa ujumla. Nafahamu , njaa ikiuma sana huyumbisha ubongo.
Tujifunze kuvumilia njaa ili nyakati za chaguzi tusiwe tunawachagua watu kwa vigezo vya wingi wa kutoa pesa za rushwa kwani tumekuwa tukichagua walio wengi ambao kamwe hawaoni wala hawajui thamani yetu ya kuwachagua wao.
leo hii kwa mfano tuitishe mikutano ya hadhara kisha tuwaambie wananchi wakae nyuma ya viongozi walio wataka wao watu wataumbuka. Basi wanaojijua wana makando kando wajirekebishe wazaliwe upya kitabia.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuandika kwenye kitabu cha tujisahihishe ukurasa 08 Ninamnukuu, "mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiria kwa makini kama viongozi hao wanaweza au hawawezi kazi wanayochaguliwa kufanya.
"wanachama wetu hufanya makosa makubwa sana ikiwa watachagua viongozi wao hovyo tu. Hili ni jambo la hatari kwa demokrasia na chama chetu. Ni wajibu wetu katika kuhifadhi demokrasia kuona kuwa tunachagua Viongozi ambao wanaweza kazi yao." Mwisho wa kunukuu
Tuache uoga tuiangalie haki na usawa mawazo hasi na ya hovyo yanatuchelewesha Nakumbuka niliwahi kusoma kitabu cha Power of Positive Thinking ukurasa 13
Mwandishi Anu Sehgal aliwahi kuandika," most of our negative habits come from parents and teachers that were negative most of the time."Tukisoma kitabu cha build yourself confidence uk 59
Maandiko yanasema," inferiority complex can be dangerous for growing individual. Such a person can never work towards greatness. He often commit mistakes in order to hide his own weaknesses."
Tukisoma maandiko kitabu cha nukuu za kiswahili za mwalimu ukurasa 165
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "viongozi wasifiche makosa , Haya ni makosa kwa kuwa njia pekee ya kusonga mbele ni kuyakabili kama yapo , kuyakubali kuwa ni matatizo na kuyatafutia njia za kuyatatua na sio kujidai kwamba hayapo."
Mwisho wa kunukuu Tukisoma kitabu cha the Magic of Thinking Big ukurasa 66
Mwandishi David J Schwartz PH D anasema, "where success is concerned, people are not measured in inches or pounds or college degree, or family background; they are measured by the size of their thinking, how big we think determines the size of our accomplishment."
Tukisoma kitabu cha Uongozi wetu na hatima ya Tanzania ukurasa wa 88 Mwalimu Nyerere aliwahi kuandika,
" wanaccm kwa vitendo vyao lazima waanze kupiga vita utamaduni wa woga na fidhuli ya viongozi." uongozi ni uaminifu na uadilifu.
Tukisoma maandiko Matakatifu kutoka kitabu cha Fadhila za Sadaqaat ukurasa 17 - 18 Maandiko matakatifu ya mwenyezi mungu yanasema, "rasulullahi swallallahu allaihi wasallam akisema ' miongoni mwa watu saba watakaofurahia kivuli cha arshi ya allah taala wakati kutakapokuwa hakuna kivuli chengine katika siku ya kiama ni kiongozi Mwadilifu. Mwisho wa kunukuu
Kiongozi bora anaguswa na hali duni na mateso ya walio wengi waliomuamini na kumpa ridhaa. Pia anaheshimu na kutii Sheria wala hatumii mamlaka yake vibaya kutisha walio wengi.
Kidumu Chama cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga