Kiongozi anasimama mbele ya umma na kujisifia kukopa! Haya ndiyo matokeo baada ya USA kusitisha misaada

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,733
4,914
Viongozi wengi wazalendo wa kweli waliopita walisisitiza juu ya Afrika kujitegemea na kuacha kutegemea mataifa ya magharibi. J.K Nyerere, Kwame Nkrumah, Thomas Sankara, John Magufuli na viongozi wengi mashuhuri waliweka msisitizo juu ya Afrika kutumia rasilimali zetu wenyewe kama vile ardhi safi, madini mbalimbali, watu nk. Katika kujiendeleza wenyewe. Leo hii taifa kama Tanzania lenye rasilimali za kila namna limeshindwa hata kuzalisha kiti cha plastic! Achilia mbali hata dawa ya maumivu ya kichwa!

Madini yote haya tuliyonayo, bado hayajatunufaisha ipasavyo, kwani hata chanzo kikuu cha mapato bado serikali inategemea kodi za watanzania masikini!

Kama yote hayo hayatoshi, anatokea kiongozi anajisifu hadharani mikopo, misaada na hisani za wazungu! Kiongozi anazurura kutwa kutafuta misaada na kuombaomba mikopo, badala ya kuwekeza nguvu katika kuzalisha wataalam na mbinu bora za kujikwamua kiuchumi!

Marekani imezuia misaada ya afya kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, Leo tunajawa na hofu kwa sababu ya viongozi wa aina hii, viongozi waliokosa maono!
 
Back
Top Bottom