KINGA YA RAIS KUTOSHITAKIWA

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
43,394
81,242
Hivi kinga ya rais ni hata pale alipofanya makosa ya jinai/civil makusudi kabisa. MFANO....(hypothetical example anyway...): Anaamulu kuwa chinja mwanamke nione mtoto anakaaje tumboni anachinjwa kwa vile ana kinga akiwa madarakani/akitoka madarakani asishitakiwe. Wajuzi wa sheria, kinga inakwenda mpaka huko?
 
Kinga ya Rais ni wingi wa Wabunge wa chama chake bungeni kama ilivyo Madaraka ya rais. Bila kuwa na wingi huo rais hata kinga inakuwa kama haipo
 
Kinga ya Rais ni wingi wa Wabunge wa chama chake bungeni kama ilivyo Madaraka ya rais. Bila kuwa na wingi huo rais hata kinga inakuwa kama haipo
Si kweli, soma katiba uielewe!
Ibara ya 46 sehemu ya (1) ya Katiba inasema wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

Sehemu ya (3) inasema isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A (10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.

Ibara ya 46A sehemu ya (1) inasema bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

Sehemu ya (2) imeweka masharti kwamba bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais; (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20 (2) ya Katiba.

Mbali ya Katiba ya sasa kumwekea kinga Rais mstaafu, Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba na Katiba Inayopendekezwa zilinakiri kipengele hicho kinachompa Rais mstaafu kinga ya kutoshtakiwa bila kubadili chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…