Kinachotisha ni nyama na damu sio mifupa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
311,030
763,200
Nadhani si mara moja au mbili umepata kuona onyo la picha au picha mjengeo kwamba zinatisha..

Tulisoma na kijana mmoja aliyenusurika mauaji ya kimbari Rwanda mwaka 1994.. Alikuwa amepata trauma ya kuweweseka kila wakati... Simulizi yake inatisha sana

Kipindi kile cha mauaji alishuhudia watoto mitaani wakichezea vichwa vya watu mitaani kama mpira.. Lakini kitu kilichomuacha na trauma isiyosahaulika ni siku aliyoshuhudia Intarahamwe wakichinja familia yake yote ya watu 6, dada wawili kaka wawili na wazazi wote wawili

Wakati wauaji wanaingia uwanjani kwao yeye alikuwa chooni hivyo alichomoka na kupanda juu ya mti uliokuwa nyuma ya nyumba yao na kushuhudia kwa macho yake wakichinjwa mmoja baada ya mwingine
Aliishi kwenye ule kwa wiki nzima.. Usiku akishuka na kuingia ndani kupata chochote huku ndugu zake wakioza uwanjani anawaona bila msaada wowote..

Baadae alipata msaada na kukimbilia Tanzania na baadae nje ya nchi.
Hakuondoka na chochote.. Hakuwazika ndugu zake..😭

Picha za namna hiyo zilikuwa ni nyingi na za kutisha sana zisizoangalika... Lakini baada ya nyama zote kuoza na kwisha kabisa.. Yalibaki mafuvu na mifupa ambayo ilikusanywa na kuwekwa kwenye makumbusho
Kwasasa watu wanatembelea hayo makumbusho ya kuiangalia bila hofu kubwa...

Kumbe binadamu si kitu baada ya damu kukauka, nyama kuoza na kupotea na kubaki mifupa tuu... Mnamkumbuka Rama mla watu?
Kuna watu wengi tu wanamiliki mafuvu na mifupa ya marehemu wakiwepo wafanyabiashara, watu maarufu, viongozi wa kisiasa na waganga wa kienyeji.. Swali la kujiuliza waliipata wapi? Ilikuwa mifupa na mafuvu tupu ama na nyama zake?
warning-disturbing-content-viewer-discretion-260nw-1060794641.jpg
 
Back
Top Bottom