Kinachomkuta Harmonize kurudiana na Kajala si kipya katika ulimwengu wa mapenzi

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,528
3,342
Ahlan wa Sahlan

Katika kuperuzi mtandaoni nimekutana na habari zinazotrend zinazomuhusu mwanamuziki Harmonize aka Bakhresa kuwa anapigana juu chini ili aweze kurudiana na muigizaji Kajala.

Kwa haraka haraka mtu anaweza kusema kuwa Harmonize anatafuta kiki ili atrend mitandaoni ila kwa jicho la mbali ukitazama unaweza kuona kuwa hiyo sio kiki ila kijana Bakhresa ameleweshwa kimapenzi na huyo Milf (Kajala).

Harmonize amejitahidi kuukimbia ukweli wa kimapenzi kwa kwenda zake kuanzisha penzi jipya na mwanamke kutoka Australia ila bado moyo wake umekataa kusonga mbele, badala yake umebaki katika gereza la Kajala.

Mwanaume kuna kipindi unaweza ukapita kwa wanawake wengi ila ukanasa katika tundu bovu la mwanamke mmoja na hapo ndio utajikuta huchomoki maana moyo umeshanasa.

Kabla ya kusema kuwa ni kiki, tujiulize Harmonize alipewa nini na huyu mwanamama Kajala kiasi moyo wake umeshindwa kusonga mbele??

Harmonize tayari ni star mkubwa Tanzania na Africa kwa ujumla, hivyo haihitaji kiki za Kajala ili mziki wake usonge mbele.

1648626263641.png
 
Kuachwa na mwanamke ambae bado ulikuwa unampenda huwa kunauma sana. Mwanaume unaweza kufanya lolote ili kuwin back penzi lako.

Muulizeni DeepPond na mchepuko wake ,jinsi gani alivyokwenda kupasua vioo vya gari vya jamaa alieingilia penzi lake na mchepuko.
Angekua anampenda asingetokoza Mwanawe in short K ni paka mapepe ila Konde ni kichaa!!na hamrudii ng'odo maana sio type yake

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Huyo manzi alimsumbua sana Majani miaka ile.

Walipoachana produzer alipoteza hata focus ya kupiga midundo pale BR na akatoa songi la kuomba sorry akiwa na Dully nadhani ilikuwa inaitwa Please forgive me.

Yani majani na ubabe wake wote alikuwa mnyonge sana na kuomba sana misamaha akaenda chora na matatoo mikononi ili kujifariji lakini manzi alikaza mbaya.

Nahisi huyu Konde asipotuliza akili anaweza akaharibu kazi kama manzi hatarudisha moyo nyuma.
 
Back
Top Bottom