Hawa akina mama wanafanya kazi ngumu saana na huenda kwa ujira mdogo pia. Wengi wao ni watu wazima.Kwanza ni nani amewaajiri hawa? Kufanya kazi katika mazingira yale ni hatari saana kwa afya zao, maana muda wote wapo kwenye vumbi. Lakini pia vyombo vya usafiri ni hatarishi kwa maisha yao na lile jua, uwezekano wa kupata kansa ya ngozi unaongezeka.
Swali la kujiuliza, siku hizi kuna magari maalum yanayoweza kufagia barabara kwa ufanisi. Kuna sababu gani kuwatumia watu hawa katika hii kazi? Lakini pia wale ambao si waaminifu hupeleka michanga katika mifereji. Licha ya kwamba watu hawa wanahitaji ajira lakini wanahatarisha mno maisha yao. Watu wa OSHA wanaishia wapi?