Kilwa: Jeshi la Polisi lapiga marufuku Mkutano wa Hadhara wa ACT Wazalendo kwa Sababu za Kiusalama

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,418
3,620
Mkutano wa hadhara wa Chama cha ACT Wazalendo uliotarajiwa kuhutubiwa na Kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu ambao ulipangwa kufanyika katika viwanja vya Maalim Seif Garden, Kilwa Kivinje, mkoani Lindi leo, Ijumaa Desemba 06.2024 umepigwa marufuku na Jeshi la Polisi kwa kile kinachoelezwa kuwa uwepo wa taarifa za kiintelijensia za uvunjifu wa amani

Barua ya Jeshi la Polisi iliyotumwa kwa Katibu wa ACT Wazalendo (W) Kilwa imeeleza kuwa baada ya Jeshi hilo kujipanga vyema katika kuimarisha ulinzi na usalama ndipo mkutano huo utakaporuhusiwa

Barua hiyo ya Jeshi la Polisi ambayo imesainiwa na ASP Godluck J. Munis kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Kilwa, ambayo pia imetumwa nakala zake kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Lindi, Mkuu wa wilaya ya Kilwa na kwa DSO Kilwa imebainisha kuwa kwa sasa chama hicho kinaruhusiwa kufanya kikao cha ndani kwa tarehe husika

"Angalizo; zingatia utii wa sheria bila shuruti kwani kwenda kinyume na katazo hili hatua kali za kisheria kwa kiongozi/ viongozi na wafuasi ambao watakiuka katazo hili" -imeeleza sehemu ya barua hiyo.

1733479902515.png
 
Kazi ya Bibi wa Kizimkazi na serikali yake isiyo jiamini!!

Kwa hiyo na Usalama wa Taifa wameingizwa kwenye ligi!

Aibu kwa Rais Samia!
 
Intelijensia kali sana hiyo! Inaweza kuzuia tu mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani lakini si kukamata wavunjifu wa amani kwenye mikutano ya hadhara!
 
Back
Top Bottom