Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa vyanzo vingi vya maji na ardhi kubwa na yenye rutuba Kutokana na ufinyu wa ajira juu ya vijana wetu waliomaliza vyuo na kubaki majumbani wakisubiri ajira, serikali kupitia wizara yake ya kilimo ingetumia nguvu kubwa juu ya vijana kujikita katika kilimo cha kisasa cha umwagiliaji na chenye faida kubwa kuliko kilimo cha kutegemea mvua ambacho unaweza lima mvua ikanyesha isitosheleze mazao kukomaa au ikanyesha nyingi na kuharibu mazao
Serikali kupitia wizara ya kilimo pia ingewawezesha vijana kwa kuwakopea vifaa vya kilimo kwa gharama nafuu na kwa riba ndogo ili iwe ni chachu kwa vijana kuwa na moyo wa kufanya kilimo kwa moyo
Pia serikali kupitia wizara ya kilimo iweze kutoa mbegu na mbolea ya ruzuku kwa wakati na bila ubaguzi
Pia wizara ya kilimo wawe karibu na wakulima hao kipindi chote cha ulimaji ili iweze kuwapa mafunzo zaidi na uelewa juu ya kilimo cha umwagiliaji
Kwa kufanya hivi serikali itakuwa imeokoa mambo mengi juu ya taifa hili
Kwanza ni kuondoa wimbi la vijana wasio na kazi mtaani
Pili ajira zitakuwa ni nyingi kwani tuna maeneo makubwa ya kulima
Tatu pato la taifa litakuwa kwani liliwakopea na kwakuwa walifanya kilimo cha uhakika cha umwagiliaji basi uhakika wa ulipaji mkubwa na
Pia wakipata mazao mengi yatauzwa hadi nje ya nchi na kodi italipwa vizuri.