Irrigation Potential Lake Victoria, Tanzania – FutureWater
Utafiti ulishafanywa tokea mwaka 2008 sijui kiliendelea nini.
Kuna mmarekani alipitia maeneo ya ziwa anasema ziwa Victoria liko katika mwinuko na ingewezekana kutengeneza mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji maji. Jitihada za kumuelewa mabwawa hayo yangekaaje hazikufanikiwa labda wenye fani yao wataelewa alikusudia nini?
Kama sikosei huko kanda ya ziwa ndio Magufuli aliwaambia watu wasitegemee ndizi tu wawe wabunifu kulima mazao mengine. Ingekuwa vyema kutumia vyanzo vya maji na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji.
Mto Ruaha ndio unakatiza katikati ya Tanzania na wenyewe ungefaa pia katika umwagiliaji maji mazao bila ya kuyasahau maziwa makuu mengine kama Lake Tanganyika na Nyasa.