Ndio unaweza kulifanyia survey na ukapata hati. Kama shamba lako liko ndani ya mipaka ya mji huwezi kupata hati ya shamba, utashauriwa kupima viwanja.
Kuna hati mbili, ya kimila na ile kubwa. Kama ni ile kubwa, ni mpaka eneo husika liwe lina mpango wa matumizi bora ya ardhi. Ukithibitisha kuwa eneo lako liko mahali sahihi, linakuja suala la mamlaka iliyopo pale, kama ni kijiji au halimashauri, itabidi uwaone wakupe go ahead ili uende kwa Bwana ardhi wa eneo husika. Kiufupi, anza na Bwana ardhi, ili akuchukulie coordinates za eneo lako na aweze kuangalia kwenye master plan. Akishahakikisha kwenye master plan ya eneo husika atakwambia pa kuanzia ili uokoe usumbufu.
Hati ya kimila inazingua sana kwenye mikopo.
Mashamba yote yapo mbali na mji, kama shamba lipo mjini, ujue linaweza kupata kikwazo cha kupimwa kama shamba. Shamba likiwa kwenye barabara linapata thamani zaidi.