Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,724
- 4,475
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi, amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, lengo lake kuu ni kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati, hasa kwa wananchi wanyonge.
Maswi, alikuwa akizungumza Januari 29, 2025 katika mkoani Kilimanjaro, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, uliofanyika viwanja vya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Moshi Mjini.
Amesema katika kipindi cha utekelezaji wa kampeni hiyo, kazi kubwa zitakazofanyika ni kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya kisheria, utawala bora, elimu ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, usimamizi wa mirathi na urithi, haki za ardhi na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, haki za binadamu na wajibu yakiwemo pia masuala ya ndoa.
Amesema kazi zingine ni kutoa ushauri nasihi na huduma za kisaikolojia kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia, kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwenye sehemu za vizuizi kama magerezani na katika vituo vya polisi, sehemu zenye mikusanyiko kama sokoni, minadani, shuleni na vyuoni.
Source: Nipashe