Kilichonipa huzuni kuu kwenye iftari ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Makonda

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
9,250
16,176
Nilipata nafasi nikahudhuria tafrija hiyo fupi iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha ,
Kuna mambo machache sana nilijionea yaliyonitoa machozi Kwa muda mfupi niliokaa hapo.

Kwanza kabisa watu waliokuja kupata iftari wengi wao walikuwa watu wa kawaida au tunaweza sema watu wa hali ya chini walikuwa wengi kuliko watu wa hali ya kati na juu

Watu wengi sana walitembea Kwa miguu umbali mrefu kilomita zaidi ya 8 kutoka maeneo tofauti touti makwao kuja kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa ambazo zipo katikati ya jiji kuja kufuturu TU. Na wengine waliomba nauli za kurudi kutoka watu mbali mbali walokuwepo hapo maana walikuwa hawana chochote.

Kilichoniliza zaidi wengi wao walikuja na makontena ya vyakula yaani zile bakuli zenye mifuniko yake Kwa kificho ambapo walibebea futari Kwa ajili ya watoto wao majumbani ,maana nilisikia wakisema ya kuwa nyumbani kulikuwa hakuna chochote na watoto walikuwa wamekunywa uji TU wakati wa kufuturu hivyo wazazi walisubiriwa warudi na chakula.

Kuna ambao walikuja na mifuko midogo midogo pia kwa kificho hivyo baada ya kufuturu Kwa haraka walienda kuunga foleni upande mwingine ili wabebe pia chakula maana baada ya kuongea nao walisema nyumbani hali ni ngumu sana na kulikuwa hakuna kilichopikwa Kwa hiyo hicho chakula walichobeba Kwa kificho ndio tegemeo la nyumbani Kwa usiku huo na kuwa kinasubiriwa familia ikafuturu na hapo tayari muda ulikuwa unaelekea saa tatu.


Wengi wa wanawawake waliokwepo na waliobeba vyakula Kwa Siri Kwa muonekano wao TU wa nje hakika miili yao imechoka Sana Kwa kupigwa na maisha maana hata sura na mavazi Yao hayana Nuru kabisa.

Jobless wengi pamoja na watoto wa mtaani pia walikuja Kwa wingi Kwa maana ilikuwa ni fursa muhimu sana kwao kubadilisha chakula

Wakina mama walio wengi ndio waliobeba chakula kwenye mapochi Yao na mifuko kupeleka watoto.

Kila mtu alitafuta namna ya kuficha chochote kitu ili mradi kifike nyumbani maana niliona wanaume wengine wakificha vitumbua na maandazi kwenye mifuko y suruali

Wasiofunga na wenyewe walikuwepo sana TU Kwa madai kuwa hali ngumu nyumbani kwa hiyo hiyo ilikuwa fursa ya Peke yake Kwa siku hiyo..

Sijui serikali ifanyeje kuwaokoa watu wa hali ya chini angalau hata Kwa mlo Moja kila siku ingewasaidia wengi.
IMG_20250327_182131.jpg
 
Hali imekuwa ngum sana kipindi hii, najiuliza miaka 30 ijayo nchi hii itakuwa na Hali gani na wananchi wake. PM kumejaa vijana wanalia njaa wanaomba hata buku ya kujsave mlo, unaweza dhani ni masihara ila ukweli ndio huo Hali ni ngum mtaani si kijijini wala mijini mambo ni magum uhitaji wa pesa kuendesha maisha umekuwa ni mkubwa na pesa yenyewe haipatikani
 
Sijui serikali ifanyeje kuwaokoa watu wa hali ya chini angalau hata Kwa mlo Moja kila siku ingewasaidia wengi.
Serikali ianzishe mfuko wa jamii kusaidia kaya masikini kama wanavyofanya baadhi ya mataifa hasa barani Ulaya na baadhi ya mataifa ya kiarabu.
Mfuko huo ugharamie posho inayotosheleza mahitaji ya chakula ya familia kila siku.
 
Back
Top Bottom