Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,387
- 38,663
Walianza zamani kuonesha wao wako mbele kisiasa walipoitoa KANU madarakani na KANU ikakubaliana na matokeo.
Sisi mpaka sasa CCM Bado inasema yenyewe ikitoka madarakani nchi itaingia vitani.
Wakaja wakabadili Katiba yao na wakabadili kabisa mfumo wao wa Serikali. Tukawasifia.
Sisi hapa bado CCM inasema kuwa Katiba haileti Barabara, chakula au ajira. Tumetulia.
Wakaweka mfumo wa kupata majaji na uundaji tume ya uchaguzi tofauti kabisa na wa kwetu sisi. Tukawasifia.
Mahakama yao Kuu ikafuta uchaguzi wa Rais na kuamua uchaguzi urudiwe. Tukawasifia.
Sisi hapa mahakama yetu inatangatanga mwaka wa tatu sasa kuamua tu kama Kina Halima Mde na wenzake wako bungeni kihalali ama la. Fikiria kama mahakama yetu inaweza kufuta uchaguzi wa Rais.
Mara mara Mbili chaguo la Marais waliopo madarakani lilikataliwa na wakenya. Sisi hapa anayekuwa madarakani hatuwezi kumpinga.
Kila siku kazi yetu itakuwa kuwasifu wakenya Kwa maamuzi ya kisiasa.