kiredio Jr
JF-Expert Member
- Jul 8, 2024
- 1,028
- 1,913
Siku hiyo nilienda msibani ambapo nilifiwa na mjomba wangu, sasa kama unavyojua kwenye msiba ndugu mbalimbali hukutana. Na siku hiyo alikuwepo ndugu yangu ambaye alikuwa ni binti mrembo sana na tunafahamiana na kiukweli huwa namtamani sana.
Wakati shughuli za mazishi zimekamilika, tukabaki ndugu tu na watu wengine walitawanyika, sasa nikabanwa na haja ikabidi niende msalani, kufika msalani naingia tu nakutana na kitu kizito yaani mzigo 💩 umeshushwa na kuachwa bila kusafishwa na maji hakuna. Na niliona kabisa ni mzigo mpya usio na muda mrefu.
Nikaona isiwe tabu acha nitoke nikatafute ustaarabu mwingine, ile natoka tu namuona yule mrembo naye anakuja njia ya msalani, tukapishana na moja kwa moja akaelekea msalani na najua alichokiona alidhani tu ni mimi nimeacha ule msala pale kwenye sink.
Kuanzia siku hiyo sitamani hata kukutana tena na yule binti, kila nikikumbuka najihisi niliingia aibu kubwa ambayo kiukweli sikustahili.