Kila nikiiwaza Tanzania sipati jibu

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,235
16,205
Wakati mwingine mpaka kichwa kinauma
Mawazo ni mengi juu ya kile kinachotokea leo au kesho katika nchi
Magufuli na TRA wamekua ni jipu wanajikadiria tu kodi bila kujiuliza huyu mtu ndio anaanza biashara
Sasa kama kuanza tu biashara ni 300000 je hii ndio hapa kazi tu
Kwa mtindo huu vitu kupanda bei tanzania itakua kawaida sana
Na watu kutokulipa kodi itazidi kuongezeka bado najiuliza kama mwekezaji wa kigeni anapewa miaka 5 ya msamaha wa kodi vipi kwa mzawa anaeanza biashara leo huku akilazimishwa kulipa kodi haraka iwezekanavyo baada tu ya kuanza biashara
Hapa hakuna huruma kabisa juu ya raia wa tanzanzania hasa wale wa hali ya chini
Itafika mahali kodi itakua kama chumba cha kupangisha tu
Kila mwaka utakadiriwa kwa jinsi wanavyotaka TRA bila kuzingatia ni lini mtu ameanzisha biashara
 
Hii kodi ya anae anza biashara ilikuwa laki 2 bila kupungua uilipe TRA ndio upewe clearance uende ukapatiwe leseni, sasa kama amefuta ada ya elfu 20 halafu huku aongeze laki moja nzima, kweli ni ujuha na kuna watu wanashangilia mapato TRA yameongezeka kumbe wanao umia ni wananchi kwa kodi kuongezwa kiholela. tutakoma kuishi na kuzaliwa Tanzania.
 
Kiukweli maisha yanazidi kua magumu hakuna afadhali kabisa
 
Sijui ni kwanini hawalioni hili wao wanajua kuongeza mapato tu na kuongeza kwenyewe ndio huku hakika ni maumivu tu
Serikali haiwezi kuongeza mapato kwa kutoza kodi biashara ambazo hazina mapato ya kutosha.

Inabidi serikali iweke mazingira mazuri ya kiuchumi ya kuongeza uzalishaji na mapato kwa wafanyabiashara kabla ya kutoza kodi.

Kutoza kodi kubwa kwa biashara ambayo hata haijaanza hakuongezi mapato kwa serikali, kunapunguza mapato.Kwa sababu watu wengine wataacha kuanzisha biashara - au kuanzisha biashara kwa mfumo rasmi- kwa kutotaka kulipa kodi kubwa kabla ya kuanza biashara.

Katika somo la kodi, moja ya kanuni ya kodi ni kutowatoza watu kodi ya juu sana. Matokeo ya kuwatoza watu kodi ya juu sana ni kukosa mapato, kwani watu wataacha kufanya au kusajili biashara zao.
 
Harafu cha ajabu wafanyabiashara wakubwa hawalipi kodi kabisa...mfano kituo cha mafuta cha GAPCO kilichopo katikati ya dodoma mita chache tu toka ofisi za tra mkoa wa dodoma hawatoi risiti na ukilazimisha upewe risiti wanakupa iliyoandikwa kwa mkono ina maana zile mashine hawajapewa?
 
Sasa hilo somo na kinachotendeka hivi sasa ni vitu viwili tofaut ukifika kwenye ofice za tra ndio utaniamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…