Kila mtu yupo na maudhi yake hivyo weka mipaka ya mazoea baina yako na watu wengine ili uishi kwa kuheshimika

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,611
Watu wengi sana wanalalamika mara utasikia "siwezi kumuamini mwanaume/ Mwanamke maishani mwangu" , mwengine anasema binadamu wabaya,wengine wanasema "usimuamini mtu yeyote " n.k lakini uhalisia wa kauli hizo ni chimbuko lenye maumivu ndani yake.

Watu wengi wakipenda huwa wanasahau kwamba unaempenda ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, baadhi ya watu wakimchukia mtu huona mabaya tu ya mtu wanaemchukia lakini uhalisia ni kwamba hakuna binadamu yeyote duniani ambaye ni mzuri kwa 100% au mbaya kwa 100%,hakuna binadamu muovu kwa 100% au mwema kwa 100%.

Kila mtu yupo na mema na mabaya yake,kila mtu yupo na sifa nzuri na mbaya.

Kwa kuzingatia hilo ni kwamba hata wenye kusifiwa sana kwa wema wapo na mabaya yao na vilevile hata wenye kusemwa vibaya sana wapo na mazuri yao.

"Tumeona mabaya kwa watu wazuri na tumeona mazuri kwa watu wabaya ,tumeambiwa uongo na watu waaminifu na tumeambiwa ukweli na watu waongo, tumeshuhudia usaliti kwa watu waaminifu na tumeshuhudia uaminifu kwa watu wasaliti,tumepewa msaada na watu wabinafsi na tumenyimwa MSAADA na watu wakarimu "

Kwa kuichambua nukuu hiyo leo tuangalie namna nzuri ya kuishi na watu wengine katika jamii bila "Stress"

KILA MTU YUPO NA MAUDHI YAKE YA HAPA NA PALE
(everybody hurts sometimes"
Hakuna mtu ambaye ni rahisi kuishi naye ,kila mtu yupo na maudhi ya hapa na pale,wapo huleta maudhi wakati wa chakula,wapo huleta maudhi wakati wa mazungumzo,wapo huleta maudhi kwenye matumizi ya fedha,wapo huleta maudhi kwenye kutimiza ahadi,wapo huleta maudhi katika utendaji kazi wao,wapo huleta maudhi katika kutunza muda,wapo huleta maudhi kwa kurudia makosa mara kwa mara,wapo huleta maudhi kwa namna wanavyolala,wapo huleta maudhi kwa kufanya mzaha muda wote,
wapo huleta maudhi kwa namna wanavyodai haki zao,wapo huleta maudhi kwa kung'ang'ania vitu,

wapo huleta maudhi kwa sababu ya ugumu wa kuelewa vitu rahisi,wapo huleta maudhi kwa kufanya maamuzi bila kufikiria madhara ya matendo yao.

Kwa ujumla hakuna binadamu yeyote ambaye hana maudhi kwa 100%

Yupo anayefanya maudhi kwa makusudi muepuke,yupo anayefanya maudhi kwa nia nzuri ya kukufurahisha mueleweshe,yupo anayefanya maudhi kwa bahati mbaya mvumilie.

Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukubaliana na mawazo yako yote kila siku.Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kupokea simu zako kila siku,hakuna mtu ambaye anaweza kukufariji kila siku ukimuhitaji,hakuna mtu ambaye anaweza kuonyesha uso wa furaha kila siku ukiwa naye.

Tarajia yafuatayo kutoka kwa watu waliokuzunguka. Kwani baadhi yao
Baadhi ya watu watakosa shukurani hata kama huwa unawashukuru kila siku

Baadhi ya watu watakusema vibaya sana nyuma ya mgongo hata kama utakuwa unawasema vizuri kila siku

Baadhi ya watu watazusha uongo juu yako hata kama utakuwa muaminifu kwao miaka yote
Baadhi ya watu watafanya makosa makubwa sana yenye kukutoa machozi hata kama siku zote huwa unakwepa kuwakosea

Baadhi ya watu watapoteza hisia juu yako hata kama upo na hisia kali sana juu yao siku zote

Baadhi ya watu watafanya maamuzi kwa jazba hata kama huwa haufanyi maamuzi kwa jazba dhidi yao

Baadhi ya watu watakufokea hata kama utakuwa hauwezi kufanya hivyo kwao

Baadhi ya watu watavujisha siri zako hata kama huwa unatunza siri zao miaka yote
Baadhi ya watu watapuuza simu zako hata kama simu zao unazipa kipaumbele kila siku.

Tarajia baadhi ya watu watabeba chuki na kinyongo dhidi yako hata kama hauna chuki wala kinyongo dhidi yao

Tarajia baadhi ya watu watakwamisha kazi zako kwa makusudi hata kama huwa unajitoa mhanga kuwafurahisha katika kazi zao kila siku.

Tarajia baadhi ya watu watakusaliti hata kama utakuwa muaminifu kwao miaka yote
Tarajia baadhi ya watu watakudanganya taarifa zao hata kama huwa unawapa taarifa zako sahihi kila siku.

Tarajia baadhi ya watu watashusha thamani mafanikio yako hata kama huwa hauwezi kufanya hivyo kwao.

KUWEKA MIPAKA BAINA YAKO NA WATU WENGINE ILI USIVUNJIWE HESHIMA
Unapoweka mipaka baina yako na wapendwa wako kama wazazi, walezi, ndugu,jamaa, marafiki, wafanyakazi, mwajiri, mwalimu wako, kiongozi wako wa dini, wateja, mshauri wako,mwenza wako,mfano bora wa kuigwa (Role model),jirani, wanafunzi wenza . Zingatia kwamba utajenga mazoea nao lakini mipaka ni muhimu iwepo.

Unatakiwa kujua tabia gani unaweza kuzikubali na tabia gani haupo tayari kuvumilia kutoka kwao.

Lazima Watu wengine wajue kwamba kuna makosa unaweza kusamehe vilevile yapo makosa ambayo hauwezi kusamehe badala yake utafanya maamuzi magumu bila kujali maoni ya jamii kwako yatakuwaje.

Kuweka mipaka inasaidia kuzuia watu wengine kujenga tabia ya ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji,dharau, majivuno, kiburi,dhihaka,kutaka kukutumia kwa maslahi binafsi,kuzuia baadhi ya watu ambao wanaweza kukulazimisha uhatarishe uhai wako kwa lengo la kuwafurahisha na kuwathibitishia kama unawapenda kwa dhati.

Yapo mambo siyo ya kuvumilia hata kidogo haijalishi utakuwa ûnampenda sana mtu mwengine unatakiwa kufanya maamuzi magumu mambo hayo ni kama vile -Kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa, kugombezwa, kukaripiwa, kupelekeshwa, kutolewa dosari za muonekano,kutaniwa utani wenye dhihaka na udhalilishaji, kukashifiwa imani ya dini yako,mtu unaempenda sana anapowatukana wazazi wako, kushambuliwa kwa maneno makali sana,kufanywa kichekesho haya siyo mambo ya kuvumilia hata kidogo.

Kama utakuwa hauna ujasiri wa kufanya maamuzi magumu utasababisha Watu ambao hawana heshima kwako kujenga urafiki na wewe, utasababisha Watu kuishi huku wapo na tabia ya ubabe, kiburi, majivuno, jeuri, dharau,watakutumia kwa maslahi binafsi,watakupanda kichwani,watafanya makosa makubwa sana kwa makusudi kabisa kisha wanageuza kibao kwako,

Watafanya makosa makubwa sana kwa sababu wanaona hauna MADHARA yoyote kwao .
Hivyo upole , huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa kutaonekana kama UDHAIFU wako kwao.
 
Simamia kile unachokiamini, keeping in faith kwa Mwenyezi Mungu unayemwaamini akuongoze vyema wakati wote wa maisha yako. Kama unachokifanya nafsi yako haikusuti hata chembe endelea, ukifanya kwa muda mrefu utashangaa mambo yanapokuja pamoja., Ili uwe mtu bora sahau juu ya kisasi, haijalishi ni kwa namna gani ulipondwa., ji_evaluate. Hakuna fundi wa kuishi wote tunajifunza. Acha Dharau.
 
Utakuta mtu anakomaa kusema Trust nobody! Trust nobody! Trust nobody!

Halafu na yeye asipo aminiwa anaanza kudhani anadharauliwa au kunyanyapaliwa.

Anasahau kwamba kwenye hiyo "Nobody" na yeye yumo.
 
Back
Top Bottom