Kikwete: Uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu na Ujenzi wa Ikulu haukuwa wa mtu mmoja!

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,484


Heshima kwenu Wakuu wangu,

Leo Taifa tumeweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.

Ikulu ambayo itafanana na ile iliyopp Dar Es Salaam kwa kila kitu hadi upana wa ngazi. Tofauti ni moja tu kwamba ile ya Dodoma ina underground.

Lakini katika waliohutubia, Makongoro Nyerere na Jakaya Kikwete ndo wamefanya watu kusahau machungu ya maisha na hasira za Corona kwani wamechangamsha Ukumbi japo hata ambaye hakucheka alitabasamu kwa furaha.

Rais Mstaafu Kikwete alipo simama kuhutubia alianza na neno "Mambo"? Nikaona kila mtu hata wale Maafande wa JKT wanaojenga Ikulu wakavua kofia na kuepeperusha hewani kwa shangwe na Vifijo.

Kwenye hotuba ya rais Mstaafu Jakaya Kikwete nimegundua hili:

1. Kikwete ameshangiliwa sana na vijana wa JKT kuliko rais yoyote mstaafu

2. Kikwete amezungumzia kuwa Mwalimu hakuamua tu Makao Makuu yahamie Dodoma yeye mwenyewe, Ulikuwa ni uamuzi wa kidemokrasia na uamuzi shirikishi. Hapa aliweka msisitizo wa uongozi shirikishi na demokrasia (collective decision-making)

3. Alieleza uamuzi wake kuwa Makazi ya Rais na ofisi zijengwe Chamwino. Mawazo ya zamani ni kuwa Ikulu ijengwe Chamwino halafu ofisi ya Rais iwe Chimwaga, hiyo isingekuwa salama Rais asafiri 40km kila siku kutoka Chamwino kwenda Chimwaga na kurudi. Hii imedhihirisha kuwa uamuzi wa kuhamia Dodoma ni mchakato ambao kila Rais alikuwa na mchango wake, siyo maono ya kiongozi mmoja peke yake.

========
Rais mstaafu Jakaya Kikwete asema kuwa anashukuru kwa kualkwa kushuhudia tukio la kihistoria ,ndoto zimetimia, amesema mwaka 1971chama cha TANU kiliamua makao makuu yahamie Dodoma na ni uamuzi uliofanywa kudemokrasia ni uamuzi shirikishi.

Baada ya kutokea hilo vuguvugu la kwamba kujengwe makao makuu katikati mikoa iltakiwa kwenda kutoa maoni na mikoa mingi ikakubali karibu yote na mkoa mmpja ulikataa ambao ni mkoa wa Pwani.

Amesema mkoa uliokataa ni mkoa wa kwao ambao ni mkoa wa Pwani na amesema isingekuwa rahisi kukubali kwa kuwa walikuwa wanatoa makao makuu kwao na kupeleka Dodoma kwa watu wengine.

Amesema ni kama vile Bagmoyo walivyosikitika wakati ule wa mjerumani walipohamishia utawala Daresalaam, amesema wakati mjerumani anatawala alikuwa anatawala kutokea Bagamoyo na ndio maana jengo la Bagamoyo lile kubwa linafanana na jengo la ikulu lakini kwa kuwa walikuwa wanataka bandari
wakaamua kuhamishia Dar es alaam.

Amesema kuwa wazo lilikuwepo wakati wa baba wa Taifa akachagua Chamwino akajenga ikulu na wakati wote wazo lilikuwa makao makuu Dodoma lakini dizaini walioitayarisha ya makao makuu ya ikulu ni pale juu Chimwaga yakajengwa makao makuu ya chama lakini pia ilikuwa ikulu inajengwa pale.

Akaendelea kusema kuwa yeye alipokuwa Rais alifanya uamzi kuwa wanataka kujenga chuo kikuu kikubwa kuliko vyote Dodoma na uamuzi huo haukuwa wa kudemokrasia maana watu walikuwa wanasema mara tujenge Mwanza mara wengine tupeleke Dodoma wengine Mtwara mara wengine Mbeya ndipo yeye akafanya maamuzi kama Rais kuwa watajenga Dodoma.

Lakini sasa wataanza vipi akasema waanze palepale kwenye jengo lile ambalo chama kinalitumia kila baada ya miaka mitano na hakuna mtu anayetumia na uzuri lilikuwa lishauzwa kwa serikali baada ya kuingia kwenye vyama vingi.

Baada ya uamuzi ule palipokuwa panatakiwa kujengwa makao makuu ya serikali ndipo pamejengwa chuo kikuu na ikulu lazima ijengwe Dodoma. Ndipo Rais mstaafu Kikwete akawambia ikulu itajengwa Chamwino ikaja mjadala lakini makao makuu inatakiwa kuwa Dodoma na Chamwino ni nje ya Dodoma akajibu kuwa Dodoma ni jina tu na Rais anaweza kuamua kuwa hapa pote kuwa ni Dodoma.

Akaamua kuwa hapo iwe manispaa na kwa mzee Marechela pakawa manispaa akasema Rais atakuwa anakaa Chamwino ikulu yake ikajengwe Chimwaga, huyo Rais atakaye kuwa anatembea kila siku asubuhi kilomita karibu 40 akaona sio salama hivyo akasema ikulu yake ikajengwe kulekule Chamwino.

Na baba wa taifa aliamua kuwa ikulu ijengwe palepale Chamwino na mipango ikaanza, na majengo ya wizara yajengwe kuzunga ikulu na sasa wamepata mtu ameifanya mipango kuwa matumizi '' Hongera sana mh. Rais, Rais nakupongeza sana uamuzi wa kujenga ikulu ni uamuzi wa busara na wa hekima''

Aliendelea kusema kuwa anaungana na wengine kupongeza na viongozi wa dini jambo hili likamilike kama ilivyokusudiwa na kama mh. rais alivyokudia na ameshangaa maendeleo kwa mambo mengi yaliongezeka na majengo mengi yaliyojengwa.

Aliendelea kusema kuwa amefurahi sana kwa kuzawadiwa ndege aina ya tausi maana alikuwa nafikiria kwenda kwa mh Rais kuomba ili akawafuge kwake Msoga. lakini amepewa kabla hajaomba hivyo amefurahi sana, na amemuomba mh. Rais ampatie masaada wa ujuzi wa kuwafuga ili wasije kufa kwa kukosa matunzo bora.
 
“Wakati Mzee Kikwete ananikabidhi Ikulu aliniambia Tausi hawa wanataga mayai vizuri ila hawayalalii yanaliwa na wanyama, kuna mfanyakazi hapa tena msukuma mwenzio kila nikimuambia atafute incubator atotoe mayai hafanyi, nilipoingia yule Msukuma nikamfukuza”-JPM
 
Kuna uzi uletwa humu ukiwa na picha la jengo wakisema ile ndio ikulu, watu wakamtukana sana Magu sasa leo wanaumbuka tena.
Kiukweli chadema ni fungu la kukosa
Hiyo ndiyo ilikuwa iwe ikulu ya Magu wakamkosoa ndipo akaanzisha mchakato wa haraka kujenga ikulu kama ya Dar. Na kwa taarifa yako ikulu imeanza kujadiliwa mwaka huu january. Kama hujui kitu kaa kimya!
 
Back
Top Bottom