Kikundi cha rsf kuongea na waandishi wa habari jijini Nairobi- kenya ikiwa ni baada ya kupoteza udhibiti wa mji wa wad madani

Strong ladg

Senior Member
Jul 15, 2021
131
340
Kulingana na The Eastleigh Voice, kikundi cha RSF cha nchini Sudan kitaongea na waandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya mnamo Jumatatu ya tarehe 13 Januari 2025. Hii inakuja ikiwa ni siku moja tangu RSF wapoteze udhibiti wa mji muhimu wa Wad Madani.
Kuipoteza Wad Madani ni pigo kubwa kwa RSF kwa sababu mji huo ni muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa silaha pamoja na bidhaa nyingine zinazohitajika wakati wa vita.
RSF walikuwa wameudhibiti mji wa Wad Madani tangu December 2023.

View: https://x.com/Eastleighvoice/status/1878668094219976870?t=7MqXRKT18xPHjgpef-2KLg&s=19

"How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army? | Sudan war News | Al Jazeera" How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army?
 
Kwanini iwe Nairobi na sio huko huko walipo?

Wana uhusiano gani na Nairobi?
 
Duh aiseee kutafutiana majanga tu huko Nairobi,wangeongelea sudan mpakan
 
Kuna post nyingine nimeona Mkenya kakomenti kwamba huyo kiongozi wa RSF anaishi Nairobi. Kataja hadi mtaa anaoishi. Kama ni kweli anaishi Nairobi, mmh. Sijui Ruto ana mpango gani . Ni jambo la ajabu
 
Hata kama ni freedoom expression lakin nadhani Nairobi inaji position in the wrong way in the region maana wapinzani wote wa kanda wanafanyia declarations zao.Nairobi
 
Kulingana na The Eastleigh Voice, kikundi cha RSF cha nchini Sudan kitaongea na waandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya mnamo Jumatatu ya tarehe 13 Januari 2025. Hii inakuja ikiwa ni siku moja tangu RSF wapoteze udhibiti wa mji muhimu wa Wad Madani.
Kuipoteza Wad Madani ni pigo kubwa kwa RSF kwa sababu mji huo ni muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa silaha pamoja na bidhaa nyingine zinazohitajika wakati wa vita.
RSF walikuwa wameudhibiti mji wa Wad Madani tangu December 2023.

View: https://x.com/Eastleighvoice/status/1878668094219976870?t=7MqXRKT18xPHjgpef-2KLg&s=19

"How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army? | Sudan war News | Al Jazeera" How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army?

Vita vinavyoendelea Africa ni ushahidi tosha kuwa African Union siyo umoja sahihi kwa bara letu.

AU ni umoja wa viongozi wa Afrika.

Ipigwe vita. Ivunjwe kisha kila nchi ipige kura ya maoni kujiunga
 
AU ni tawi la EU lenye ofisi za NATO ndani ya ofisi za makao makuu pale Addis Ababa Ethiopia. AU haina msaada wowote , inasubiri nchi fulani ifanye mapinduzi itoe kauli za kukemea na kusimamisha uanachama. Kama kuna mtu ana matumaini na AU nampa pole. Au ni kamradi kakupiga pesa na fursa ya viongozi kwenda kukutana kupiga picha na kuondoka. Hamna chochote cha maana pale
 
Hata kama ni freedoom expression lakin nadhani Nairobi inaji position in the wrong way in the region maana wapinzani wote wa kanda wanafanyia declarations zao.Nairobi
Kabisaa. Yaani unaruhusuje kikundi cha RSF kufanya mkutano kwenye nchi yako. Sijui Ruto anafikiria nini kwa kweli ? Hii ni sawa na kusikia M23 wanafanya mkutano jijini Dar
 
Mbona inasemekana Laurent Kabila alikuwa anaishi bongo huku akifanya mishe zake DRC??

Mbona inasemekana Museveni na familia yake wamewahi kuhifadhiwa bongo?
 
Kulingana na The Eastleigh Voice, kikundi cha RSF cha nchini Sudan kitaongea na waandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya mnamo Jumatatu ya tarehe 13 Januari 2025. Hii inakuja ikiwa ni siku moja tangu RSF wapoteze udhibiti wa mji muhimu wa Wad Madani.
Kuipoteza Wad Madani ni pigo kubwa kwa RSF kwa sababu mji huo ni muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa silaha pamoja na bidhaa nyingine zinazohitajika wakati wa vita.
RSF walikuwa wameudhibiti mji wa Wad Madani tangu December 2023.

View: https://x.com/Eastleighvoice/status/1878668094219976870?t=7MqXRKT18xPHjgpef-2KLg&s=19

"How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army? | Sudan war News | Al Jazeera" How strategic is Wad Madani city, retaken by Sudanese army?

Ni nani mfadhili wa hizi vita duniani? Ni wazi ni wale ambao uchumi wao unategemea silaha
 
ahmed dagalo miaka yote yupo nairobii...funding za rsf zatoka dubaii
 
Mbona inasemekana Laurent Kabila alikuwa anaishi bongo huku akifanya mishe zake DRC??

Mbona inasemekana Museveni na familia yake wamewahi kuhifadhiwa bongo?
Sio inasemekana ni ukweli mtupu. Huyo museveni hadi alitoa pesa ya kujengea familia pale Muhutwe Muleba nyumba ambapo aliishi hiyo pesa ikapelekea wanafamilia kumuua mama ambaye alikuwa ni mjane aliyepatiwa hiyo fedha. Yani mama mkwe na kaka wa marehemu ndugu zake walimchinja ili wachukue hizo fedha. Mama akafariki ni kumwacha kijana wake mmoja.
 
Back
Top Bottom