Kikundi cha Hezbollah ni nini na ilianzia wapi?

Mtanzania2020

JF-Expert Member
May 23, 2020
788
1,666
HEZBOLLAH NI NINI HASA?

Kwa haraka sana, Hezbollah ni chama cha siasa nchini Lebanon LAKINI KUMBUKA CHAMA NI CHAMA CHENYE JESHI LENYE SILAHA!

Yaani, jenga picha mfano wa vyama vyetu hapa nchini.

Sasa, moja ya vitu ambavyo ni vya kawaida sana pale Mashariki ya Kati, ni chama kuwa na jeshi kama jeshi kabisa, lenye silaha, ndege za kivita, mabomu, makombora nakadhalika.

Mpaka hapo umepata ile picha rahisi ya haraka.

Tukisema Hezbollah maana yake kwa Kiswahili tumesema 'chama cha Mungu' ambacho kinaundwa na Waislamu wa dhehebu la Shia.

Sasa, kuna maswali mengi, mfano:

Kama ni chama tu cha siasa, kwa nini kiwe na mabavu kiasi cha kupigana vita na nchi nyingine?

Sijui kama unanielewa?

Yaani mfano, tuseme vyama vyetu vya siasa hapa Tanzania viwe vina majeshi: sasa, inawezekanaje Red Brigade ya Chadema kwa mfano, iwe na mabavu ya kuanzisha vita dhidi ya Kenya? JWTZ watakuwa wako wapi? Red Brigade watakuwa wanatolea wapi huo 'ubavu' wa kupigana na nchi nyingine kama Hezbollah inavyopigana na Israeli mara kwa mara?

Jeshi rasmi la nchi ya Lebanoni linasemaje na serikali kwa ujumla?

Lakini kuna swali la pili: Hezbollah anapata wapi nguvu za kuwa na jeshi kubwa na imara la namna hii?

Wanapataje pesa za kujiendesha kiwango cha kutumia matrilioni ya fedha kununua silaha, kugharamia jeshi, na kugharamia vita?

Hebu kwanza tujibu haya maswali kwa kueleza historia fupi kabisa ya Hezbollah.

Siku ya Alhamisi, tarehe 3 mwezi June mwaka 1982 katikati ya jiji la London Uingereza, kulitokea tukio lililokuja kuleta mlolongo wa matukio makubwa ulimwenguni ikiwemo kuundwa kwa chama hiki cha Hezbollah.

Vijana watatu, Hussein Ghassan Said, Marwan al-Banna, na Nawaf al-Rosan walimvamia aliyekuwa Balozi wa Israeli nchini Uingereza akiwa ametoka kwenye sherehe iliyofanyika kwenye hoteli iliyoitwa Dorchester iliyopo mtaa wa Park Lane hapo London.

Hussein Ghassan alimvizia na kumsogelea Mheshimiwa Balozi Shlomo, kisha akatumia pistol yake (PM-63 machine Pistol), akamtandika Shlomo risasi ya kichwa.

Bahati iliyoje, balozi Shlomo hakufariki, lakini alikuwa ameumia vibaya mno.

Alikimbizwa hospitali, akafanyiwa upasuaji wa ubongo na hakuzinduka hadi miezi mitatu baadaye.

Vijana wale wote walikamatwa pale London, na ndipo ilipogundulika kuwa ni wafuasi wa kikundi kiitwacho Abu Nidal Organization.

Haraka, Israeli ikatangaza kitendo walichofanya vijana wale ni 'casus belli' (yaani ni tangazo rasmi la vita!)

Israeli hakiuwa inatania, kwani siku tatu baadaye Israeli ilivamia nchi ya Lebanoni kuwasaka maadui wa namna hiyo nchini humo.

Huo ukawa ni uvamizi wa pili Israeli kufanya nchini Lebanoni baada ya ule wa kwanza wa miaka michache iliyokuwa imepita, mwaka 1978.

Uvamizi uligharimu maisha ya maelfu ya watu Lebanoni, maana Israeli 'ilimwaga moto' kwa hasira kali.

Israeli walitandika Lebanoni kwa miezi mitatu, ambapo watu elfu kumi na tisa waliuawa.

Israeli wakaita vita vile 'Operation Peace for Galilee'.

Sasa basi, wakati vita vile vikiendelea, kuna kikundi cha viongozi wa dhehebu la Shia waliwaza jambo.

Walipanga kuanzisha chama ambacho malengo yake makuu yatakuwa kwanza ni KUANGAMIZA TAIFA LA ISRAELI.

Lengo la pili, KUONDOA USHAWISHI WA NCHI ZA MAGHARIBI HASA MAREKANI ENEO LA MASHARIKI YA KATI NA KUDHIBITI USHAWISHI WA SAUDI ARABIA PIA.

Tatu, KUANZISHA TAIFA LA KISHIA NDANI YA LEBANONI.

Kama utani, Hezbollah ikawa inazaliwa hivyo.

Chama hiki kilipoanzishwa kilifadhiliwa kwa kupewa msaada mkubwa na Iran.

Tangu kuanzishwa kwake hadi leo, chama hiki kikiwa kina umri wa miaka karibu arobaini, Iran imekuwa mshirika mkuu wa Hezbollah.

Kwa nini Iran?

Kwa sababu kwanza taifa la Iran ni taifa la Waislamu wa dhehebu la Shia. Lakini pia chama cha Hezbollah kilijitanabaisha kufuata siasa zile zile za Iran za Ayatola Khomeini.

Hakika Hezbollah na Iran wakashibana, wakajazwa misaada mingi sana kiasi ambacho Hezobollah imekuwa na nguvu kubwa pengine kuliko serikali ya nchi yenyewe ya Lebanon.

Fikiri kwa mfano Hezbollah ilivyoanzishwa, ilipata msaada wa wataalamu wa kijeshi wapatao 1,500 kutoka Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC)!

Kuna wakati Hezbollah huitwa ni 'nchi ndani ya nchi'.

Ukiangalia nembo ya Hebollah, moja ya alama zilizopo ni pamoja na mchoro wa bunduki, ambayo imeandikwa mstari uliotolewa kwenye Quran usemao 'Hakika chama cha Mungu kitadumu'

Tangu Hezbollah ianzishwe, imekuwa ikisuguaga na Israeli mara nyingi, kwa kuwa lengo kuu la Hezbollah ni 'destruction of the State of Israel.'

Mwezi wa tisa mwaka 2024, Israeli ilimwua Katibu Mkuu (Secretary General) wa chama hicho, Hassan Nasrallah ambaye ndiye amekijenga chama hicho na kukifanya kiwe kama kilivyo leo.

Kifo chake kimeandamana na mauaji ya viongozi wengine ambao Israeli imefanikiwa kuwa-target na kuwaua kupitia simu, (pager) na kupitia kuwadungua wanapogundua sehemu walipo.

Hadi sasa tunapoandika, bado Hezbollah hawajapata mrithi wa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho.
 
Pokea maua Yako 🌻🌻🌻🌻
 
Sasa, moja ya vitu ambavyo ni vya kawaida sana pale Mashariki ya Kati, ni chama kuwa na jeshi kama jeshi kabisa, lenye silaha, ndege za kivita, mabomu, makombora nakadhalika.
Hapa umetupiga.
Hezbollah hana silaha kubwa kama hizi ulizoorodhesha.
Pamoja na kwamba Hezbollah wana nguvu kuliko jeshi la serikali la Lebanon lakini katika vitu hawamiliki ni pamoja na Jet fighters, vifaru na silaha nyingine kubwa.

Kwanini?
Jet fighters, zitahitaji gharama za uendeshaji, zitahitaji skilled pilots, airport na air defense systems maana zipo vulnerable to enemy aerial attacks. Hivyo Hezbollah wame-opt katika silaha za kisasa ambazo ni rahisi kuzificha zisionekane na adui haswa kwenye mahandaki, majengo.
Wao hawapigani conventional wars, mbinu yao ni asymmetric na guerilla warfare, wanakutandika wanakimbia wanapotea kujificha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom