Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 123
- 135
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Deogratius Evarist Mbuya(40) mkazi wa Legho Kilema wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua Baba mkwe wake, Tibrus Camil Mneney(72).
Mbali na mauaji hayo,mtuhumiwa pia anadaiwa kumjeruhi mama mkwe wake, Beritha Tibrus Mneney (58)ambaye amelazwa kwenye Hospital ya Kilema akipatiwa matibabu.
Tukio hilo limetokea Novemba 13 mwaka huu majra ya saa saba mchana nyumbani kwa Marehemu huko Kilema.
Chanzo cha mauaji hayo kinatajwa kuwa ni kutokana na usuluhishi wa Baba mkwe na mtuhumiwa uliotokana na ugomvi baina ya mtuhumiwa na mkewe.
Taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa Leo Novemba 14,na kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro(SACP), Simon Maigwa inasema mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa anatoka nje ya ndoa baada ya mtuhumiwa kufanyiwa upasuaji kutokana na sababu za kiafya.
"Baada ya usuluhishi kushindikana mtuhumiwa alianza kumjeruhi mama mkwe wake mkono wa kushoto na baba mkwe alipojaribu kumuokoa ndipo mtuhumiwa alianza kumkata baba mkwe na kitu chenye incha Kali maeneo ya kichwani, shingoni, mkononi na kumsababishia kuvuja damu nyingi na kupelekea kifo chake", mesema kamanda Maigwa kwenye mkutano wake na waandishi wa Habari.
Kamanda Maigwa amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka na baada ya msako mkali wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi, alikamatwa akiwa amejificha kwenye jengo ambalo hawaishi watu Mali ya Revocatus Anselim Mbuya.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo anapatiwa matibabu kwenye Hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kutokana na kuwa katika hali mbaya na hawezi kuongea.
"Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospital ya Kilema kwa uchunguzi, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika"amesema kamanda Maigwa.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linachunguza tukio la kujinyonga kwa fundi magari mkazi wa Pasua Manispaa ya Moshi.
Mwili huo umekutwa chini ya mti pembeni ya uwanja wa mpira wa shule ya msingi Mandela.
Kulingana na Taarifa ya jeshi la polisi Leo Novemba 14, 2024, Marehemu ametambuliwa kwa jina la Hassan Ally Mwanga(39) na mwili wake ulikutwa na kamba ya katani shingoni.
"Jeshi la polisi linatoa Rai kwa wananchi kutoa taarifa mapema kwenye Taasisi zenye mamlaka ya shughulikia migogoro ya ndoa Ili kuishughulikiq Ili kuepusha misongo ya mawazo yanayopelekea kutoa maamuzi magumu ikiwa ni pamoja na kusababisha mauaji na kujitoa uhai", Taarifa ya RPC Maigwa imesema.
Mwili wa marehemu Mwanga aliyekutwa kajinyonga leo, umehifadhiwa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.
Mwisho.