Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,502
- 3,131
Haki ya kuchagua (au kuomba kuchaguliwa kuwa) kiongozi ni haki ya msingi ya kila mwanachama wa CCM. Haki hii ni ya kikatiba na kikanuni.
Kwa kawaida, watendaji wa chama hutangaza kufunguliwa rasimi kwa dirisha la kuchukua, kujaza na kurudisha fomu za kuomba kugombea nafasi za uongozi (kama vile Urais, ubunge, nakadhalika). Utaratibu huo humpa kila mwanachama fursa ya kutumia haki yake ya kikatiba kama ambavyo yeye anaona inafaa.
Walichokifanya hawa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM 2025 ni kubariki political shenanigans za CC na NEC bila kuzingatia haki za wanachama wengine wa CCM. Najua, kiutamaduni, wanachama wa CCM (na hata wa vyama vingine vya kisiasa elsewhere) huamua kumuachia Rais (atokanaye na chama chao) agombee bila kupingwa, iwapo ataamua kuomba kugombea kwa kipindi kingine. Uamuzi wao huo bado hukidhi matakwa ya Katiba na Kanuni za Uongozi na Maadili.
Kilichotokea mwaka huu ni ushahidi wa mapungufu ya utaratibu wa sasa wa Rais atokanaye na CCM kuwa ndiye mwenyekiti wa vikao vyote vya juu vya maamuzi. Needless to say, architects wa hizi political shenanigans ni Samia na wagombea wenzake, kwa sababu ya nafasi zao katika hivyo vikao. Kuna mgongano wa maslahi ulio wazi. Shame on them all.