Kijana wangu alifanya QT 2013, anaruhusiwa sasa kufanya NECTA 2016?

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,306
Habarini wanaJF

Nina mdogo wangu, alifanya mtihani wa maarifa yani QT mwaka 2013 na kufaulu mtihani huo.

Ambapo alitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 au 2015 lakini kutokana na matatizo yaliyojitokeza hakuweza kufanya
mtihani huo.

Naomba ufafanuzi kwa anaejua je, anaweza kufanya mtihani kidato cha nne mwaka huu (2016)?

Kama haiwezekani afanye nini ili aweze kufanya mtihani huo??

Natanguliza shukrani kwa maelezo mtakayonipa

NB; Moderators naomba uzi huu usihamishwe.
 
ndio anaweza kwa asilimia 100 cha kufanya akajisajili kwenye kituo cha kufanyia mtihani au aende hapo alipofanyia mtihani wa QT kama kutamfaa ajisajili
 
ndio anaweza kwa asilimia 100 cha kufanya akajisajili kwenye kituo cha kufanyia mtihani au aende hapo alipofanyia mtihani wa QT kama kutamfaa ajisajili
Ahsante kwa maelezo mkuu, hofu ni kuwa huu mtihani wa QT ni miaka miwili kama hutakuwa hujafanya mtihani wa kidato cha nne matokeo yake ya QT yanafutwa na itambidi kufanya tena huo mtihani ndo aweze kufanya necta kidato cha nne, na ndivyo navyosikia watu wakisema
 
Naomba mawazo yenu mlio na uelewa na hili au ni wahusika mnapitia uzi huu
 
Nasubiri michango yenu, au kama kuna mtu ana namba ya mtu wa necta anaeweza kunipa maelezo nitashukuru sana
 
ingia link hii na udownload hilo tangazo litakuelekeza necta.go.tz/view_news?id=100
 
Kwanini matokeo yafutwe? Nenda kwenye kituo cha kufanyia mitihani atapewa procedures za kufata
 
Kwanini matokeo yafutwe? Nenda kwenye kituo cha kufanyia mitihani atapewa procedures za kufata
Evelyn Salt wanasema muda wa matokeo kuweza kufanyiwa kazi kwa mtahiniwa husika ni miaka 2 tu, ila ngoja nifunge safari niende mjini posta kabisa nikapewe maelezo
 
Ila kufanya mtihani wa form four kuna namba huwa zinahitajika za form two, hata hicho unachosema kinawezekana pia kwamba namba aliotumia form two imeisha muda kwa uhakika nenda tu kituoni

Hicho ndicho nilichotaka kufahamu Evelyn Salt ahsante ngoja nitafika nipate maelekezo, ila kama itakuwa kweli muda umeisha aisee itamvuruga dogo maana inaweza kumtoa kwenye mstari kabisa wa kusoma, maana itabidi nimsihi arudie tu tena hiyo QT na mwakani kama akifaulu ndo afanye huo wa kidato cha nne
 
All the best.....
 
Mpigie Mr.Ngwada no.0713 605598 yupo posta mpya anahusika na masuala hayo ya NECTA atakupa maelezo yote
 
Last edited:
Sifa za kujisajil kufany mthn wa CSEE unakuwepo kw miak 5,
Baad y kufany mthn w QT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…