Shimbolyo
New Member
- Sep 13, 2022
- 1
- 0
KIJANA INUKA
1
Umekaliwa kitako,
Kukwepa tamaa yako,
Wewe na jamaa zako,
Wahisi maisha mwiko,
Ujana ni mlipuko,
Kijana nyosha kiwiko.
Kitamu huwa ukoko,
Kula bila chokochoko,
Unaporemba mwandiko,
Utaukosa mwaliko,
Ujana ni mlipuko,
Kijana nyosha kiwiko.
2
Leo haujahusika,
Kuendana na masika,
Kifo hakitahusika,
Ujana ukinyauka,
Wote pia malaika,
Wakuombea inuka.
Ujana huchakarika,
Ukiishia mashaka,
Uzee hunufaika,
Mipango iliyonyoka,
Wote pia malaika,
Wakuombea inuka.
3
Kusema maji ya moto,
Unaupinga utoto,
Kupoa sio msoto,
Kutokota ni ufito,
Kijana wewe inuka,
Mwanzo mwisho kuhusika.
Imani sio kokoto,
Bali kutukuza wito,
Unayesifia kwato,
Njia yako i mkato,
Kijana wewe inuka,
Mwanzo mwisho kuhusika.
4
Kipenyo chanufaika,
Pumzi inayoshuka,
Gugumio lakatika,
Katikati mwa mashaka,
Kijana wewe inuka,
Hofu yako kuikata.
Jifanyie mapinduzi,
Kuntu na yasiyowazi,
Kieleacho ni uzi,
Sindano hutweza wezi,
Kijana wewe inuka,
Hofu yako kuikata.
5
Ajira yenye utata,
Ilikulaza Msata,
Ukadondokea pua,
Kufa pasipo kujua,
Kijana haja wakata,
Utu unapouua.
Acha kuzishika kuta,
Vumbi unapokung'uta,
Msingi nanuhusia,
Kwa yote nia kutia,
Kijana haja wakata,
Utu unapouua.
6
Nini fupi? si nyakati,
Nini shida? si wakati,
Njeo zenye harakati,
Kijana humpa tiki,
Inuka kwa uhakika,
Kwa imani utafika.
Huja vingi vizingiti,
Kwa uzito wa tikiti,
Mbebaji mathubuti,
Amenogewa kijiti,
Inuka kwa uhakika,
Kwa imani utafika.
7
Kweli hauna mvuto!
Wala sura ya mnato!
Unafikiri kitoto,
Kuogopa mkong'oto,
Unapolipasha joto,
Ujana wako ni wito.
Iendako yote mito,
Bahari haina chopi,
Nani hupenda msoto,
Uliyeona ni wapi?
Unapolipasha joto,
Ujana wako ni wito.
8
Ukiulize kiatu,
Maisha hayana utu,
Ukifikisha watatu,
Dunia huwa msitu,
Usijezamia katu,
Kijana inuka kwatu.
Kijana washika kutu,
Kwa sifa za ukurutu,
Tabia ya utukutu,
Imeshamuua chatu,
Usijezamia katu,
Kijana inuka kwatu.
9
Uliyeshindwa kushindwa,
Hujafikiri kiwango,
Maumivu kwa mtendwa,
Ameharibu mipango,
Kijana wewe mpendwa,
Inuka ng'oa mpingo.
Usifikiri kulindwa,
Unapounda mzingo,
Kweli bado hujaundwa,
Usilalie mgongo,
Kijana wewe mpendwa,
Inuka ng'oa mpingo.
10
Umejisoma haraka,
Kwamba umeshanyauka,
Umejisema wanuka,
Tamati hujaifika,
Kijana jama inuka,
Hayawihayawi fika.
Umbo uliloumbika,
Si vyema kuharibika,
Sura iliyojengeka,
Nini inaneemeka?
Kijana jama inuka,
Hayawihayawi fika.
11
Uliyeenda kazini,
Hujafa u masikini,
Waitazama kwanini?
Mbeleko ya mgongoni,
Kijana wakaa chini,
Inuka toka vumbini.
Ulicheka hadharani,
Ukijilaza bondeni,
Leo kichwa kipo chini,
Kikizuga duniani,
Kijana wakaa chini,
Inuka toka vumbini.
12
Yai lilipopasuka,
Akazaliwa Abed,
Kwayo halali kufika,
Tunuku pia weledi,
Mie bado sijafika,
Bado natia juhudi.
Hakuna cha kutukuka,
Ila roho moyo budi,
Kushukuru nadhurika,
Jamii kunifaidi,
Mie bado sijafika,
Bado natia juhudi.
13
Nini unachokijua?
Kijana leo inuka,
Kweli unajitambua?
Kijana sasa tumika,
Kesho yako elezeka,
Alama ukiiweka.
Nani anajivunia?
Ujana ukikufika,
Nini unajikingia?
Kijana ukigawika,
Kesho yako elezeka,
Alama ukiiweka.
14
Walimao wvunao,
Kijana wewe si wao,
Kucha kutwa walalao,
Usiige nyendo zao,
Kijana inuka nao,
Lakini chora kibao.
Alama huwa ni zao,
Lenye manufaa ndio,
Kivuli huishi kwao,
Wapitao na wajao,
Kijana inuka nao,
Lakini chora kibao.
15
Gunia kavu la chumvi,
Hurishai bila chumvi,
Unayengojea mvi,
Kitako kalia jamvi,
Kijana simama nyoka,
Kwa morali na inuka.
Hapana isiyo kapa,
Usubi hutoa lapa,
Kijana huyu kaapa,
Kanuia kuwa papa,
Kijana simama nyoka,
Kwa morali na inuka.
16
Kijana usikimbie,
Hautavaa kiatu,
Kijana na usilie,
Taji hutaona katu,
Kijana vipige vyema,
Vita vyako ujanani,
Kijana ujitambue,
Wewe ni mwana upatu,
Kamba jining'inizie,
Kwa akili ya ubutu,
Kijana vipige vyema,
Vita vyako ujanani.
17
Kijana kushika rungu,
Usitawanye mafungu,
Jifunze kwayo mawingu,
Hayajifungi kwa pingu,
Kijana inuka ndugu,
Na kumrudia Mungu.
Usiiweke mizungu,
Hata sasa nayo tangu,
Usigeuze uchungu,
Kwa utamu wa ukungu,
Kijana inuka ndugu,
Na kumrudia Mungu.
18
Ramani ipo nyikani,
Imeshatupwa jangwani,
Tafakari maishaini,
Ulizaliwa kwanini?
Inuka sasa kijana,
Dhambi nazo kuzikana.
Unafikiri mwishoni,
Ukibweteka mwanzoni,
Maisha yako usoni,
Kwa maono ya yakini,
Inuka sasa kijana,
Dhambi nazo kuzikana.
19
Mwendo sio kuwa mbali,
Ni kuketi kwa halali,
Alivaa kanda mbili,
Na kuchechema mithili,
Kijana usikubali,
Kupumua kwa ajali.
Uliifata asali,
Shari ikiwa dalili,
Jasho la mnyonge kali,
Layanusuu makali,
Kijana usikubali,
Kupumua kwa ajali.
20
Mama aliyekupenda,
Amekwisha kukuzaa,
Hadhi gani unapenda,
Kufa ama kujizaa?
Kijana inuka winda,
Dhahama kila mtaa.
Siku moja wajilinda,
Tamutamu kukataa,
Nafasi ukivurunda,
Ujinga unautwaa,
Kijana inuka winda,
Dhahama kila mtaa.
21
Huwezi kufaidika,
Jasho kutonufaika,
Nini ulichokiweka,
Nyayo zako kuloweka?
Kijana leo chambuka,
Inuka na kamilika.
Mwanzi uliopindika,
Kwao umeshapendeka,
Jema kutopumzika,
Ukiwa waulizika,
Kijana leo chambuka,
Inuka na kamilika.
22
Moja iliyofanyika,
Kileleni yajiweka,
Kijana haujafika,
Cha msingi we inuka,
Andaa mwendo kutoka,
Kesho utanufaika.
Mti uliovunjika,
Shina liliweweseka,
Mizizi yote kung'oka,
Kifo chenyewe chafika,
Andaa mwendo kutoka,
Kesho utanufaika.
23
Kigugumizi ng'amua,
Kutokusita tambua,
Jasho unalohemea,
Chozi unapumlia,
Ujana waelezea,
Amali zisizogoa.
Jimboni uligombea,
Ili ng'ombe kumng'oa
Sifa ukajizolea,
Kumbe unateketea,
Ujana waelezea,
Amali zisizogoa.
24
Gumzo umeshajua,
Kwa kujua kutojua,
Jua linapokuchwea,
Uso wako unawia,
Kijana inuka kua,
Yaliyopita fidia.
Kivuli kilikimbia,
Kwa mwili kunyong'onyea,
Tambua unawezea,
Haifai kuchelea,
Kijana inuka kua,
Yaliyopita fidia.
25
Povu jingi mdomoni,
Umeukosa uoni,
Kula tunda unabuni,
Huu muozo wa mbuni,
Kijana wa duniani,
Inuka twende mbinguni.
Aliishi kwa huzuni,
Kusaliti tamaduni,
Jongoo kafa mtini,
Kinyonga kafa shimoni,
Kijana wa duniani,
Inuka twende mbinguni.
26
Kungwi amechepetuwa,
Kulisimamia buwa,
Hakimu yeye kanawa,
Damu nzito ya mfiwa,
Unga uliopikiwa,
Ujana unakandiwa.
Ni kijana mwenye kuwa,
Alikana kuzaliwa,
Nchi sasa amepewa,
Imani kachokonowa,
Unga uliopikiwa,
Ujana unakandiwa.
27
Vidole huvunja chawa,
Mgonjwa humeza dawa,
Mkomavu ana mbawa,
Mnyonge ye huzagawa,
Kijana si Mwanahawa,
Inuka kanga kunjiwa.
Kijana umeshagawa,
Nguvu zilizozidiwa,
Pembe bovu umepewa,
Kufa nalo wanogewa,
Kijana si Mwanahawa,
Inuka kanga kunjiwa.
28
Ngoja ya mwanahabari,
Ameipinga sheria,
Kwa tundale yu hodari,
Kula kwa kufikiria,
Ujana sio bahari,
Nzi chini katulia.
Aliliunda shauri,
Kwa chozi kujilalia,
Kijana ni mashuhuri,
Mashairi kuyatwia,
Ujana sio bahari,
Nzi chini katulia.
29
Umeukana utumwa,
Kwazo fikra waumwa,
Kifalme umetemwa,
Masikini unagemwa,
Kijana usijepimwa,
Inuka bila kulemwa.
Shambani umeshalimwa,
Mavunoni ukisemwa,
Gudulia limefumwa,
Kitako chako chechemwa,
Kijana usijepimwa,
Inuka bila kulemwa.
30
Usijependa kunyonga,
Shingo uliyoiunga,
Mithili yake karanga,
Mafuta ukayadonga,
Kijana inuka ringa,
Kilichokatika unga.
Kijana wewe machinga,
Hukumu usijepinga,
Ishi kwa ulipo mwanga,
Maisha si kuyatunga,
Kijana inuka ringa,
Kilichokatika unga.
1
Umekaliwa kitako,
Kukwepa tamaa yako,
Wewe na jamaa zako,
Wahisi maisha mwiko,
Ujana ni mlipuko,
Kijana nyosha kiwiko.
Kitamu huwa ukoko,
Kula bila chokochoko,
Unaporemba mwandiko,
Utaukosa mwaliko,
Ujana ni mlipuko,
Kijana nyosha kiwiko.
2
Leo haujahusika,
Kuendana na masika,
Kifo hakitahusika,
Ujana ukinyauka,
Wote pia malaika,
Wakuombea inuka.
Ujana huchakarika,
Ukiishia mashaka,
Uzee hunufaika,
Mipango iliyonyoka,
Wote pia malaika,
Wakuombea inuka.
3
Kusema maji ya moto,
Unaupinga utoto,
Kupoa sio msoto,
Kutokota ni ufito,
Kijana wewe inuka,
Mwanzo mwisho kuhusika.
Imani sio kokoto,
Bali kutukuza wito,
Unayesifia kwato,
Njia yako i mkato,
Kijana wewe inuka,
Mwanzo mwisho kuhusika.
4
Kipenyo chanufaika,
Pumzi inayoshuka,
Gugumio lakatika,
Katikati mwa mashaka,
Kijana wewe inuka,
Hofu yako kuikata.
Jifanyie mapinduzi,
Kuntu na yasiyowazi,
Kieleacho ni uzi,
Sindano hutweza wezi,
Kijana wewe inuka,
Hofu yako kuikata.
5
Ajira yenye utata,
Ilikulaza Msata,
Ukadondokea pua,
Kufa pasipo kujua,
Kijana haja wakata,
Utu unapouua.
Acha kuzishika kuta,
Vumbi unapokung'uta,
Msingi nanuhusia,
Kwa yote nia kutia,
Kijana haja wakata,
Utu unapouua.
6
Nini fupi? si nyakati,
Nini shida? si wakati,
Njeo zenye harakati,
Kijana humpa tiki,
Inuka kwa uhakika,
Kwa imani utafika.
Huja vingi vizingiti,
Kwa uzito wa tikiti,
Mbebaji mathubuti,
Amenogewa kijiti,
Inuka kwa uhakika,
Kwa imani utafika.
7
Kweli hauna mvuto!
Wala sura ya mnato!
Unafikiri kitoto,
Kuogopa mkong'oto,
Unapolipasha joto,
Ujana wako ni wito.
Iendako yote mito,
Bahari haina chopi,
Nani hupenda msoto,
Uliyeona ni wapi?
Unapolipasha joto,
Ujana wako ni wito.
8
Ukiulize kiatu,
Maisha hayana utu,
Ukifikisha watatu,
Dunia huwa msitu,
Usijezamia katu,
Kijana inuka kwatu.
Kijana washika kutu,
Kwa sifa za ukurutu,
Tabia ya utukutu,
Imeshamuua chatu,
Usijezamia katu,
Kijana inuka kwatu.
9
Uliyeshindwa kushindwa,
Hujafikiri kiwango,
Maumivu kwa mtendwa,
Ameharibu mipango,
Kijana wewe mpendwa,
Inuka ng'oa mpingo.
Usifikiri kulindwa,
Unapounda mzingo,
Kweli bado hujaundwa,
Usilalie mgongo,
Kijana wewe mpendwa,
Inuka ng'oa mpingo.
10
Umejisoma haraka,
Kwamba umeshanyauka,
Umejisema wanuka,
Tamati hujaifika,
Kijana jama inuka,
Hayawihayawi fika.
Umbo uliloumbika,
Si vyema kuharibika,
Sura iliyojengeka,
Nini inaneemeka?
Kijana jama inuka,
Hayawihayawi fika.
11
Uliyeenda kazini,
Hujafa u masikini,
Waitazama kwanini?
Mbeleko ya mgongoni,
Kijana wakaa chini,
Inuka toka vumbini.
Ulicheka hadharani,
Ukijilaza bondeni,
Leo kichwa kipo chini,
Kikizuga duniani,
Kijana wakaa chini,
Inuka toka vumbini.
12
Yai lilipopasuka,
Akazaliwa Abed,
Kwayo halali kufika,
Tunuku pia weledi,
Mie bado sijafika,
Bado natia juhudi.
Hakuna cha kutukuka,
Ila roho moyo budi,
Kushukuru nadhurika,
Jamii kunifaidi,
Mie bado sijafika,
Bado natia juhudi.
13
Nini unachokijua?
Kijana leo inuka,
Kweli unajitambua?
Kijana sasa tumika,
Kesho yako elezeka,
Alama ukiiweka.
Nani anajivunia?
Ujana ukikufika,
Nini unajikingia?
Kijana ukigawika,
Kesho yako elezeka,
Alama ukiiweka.
14
Walimao wvunao,
Kijana wewe si wao,
Kucha kutwa walalao,
Usiige nyendo zao,
Kijana inuka nao,
Lakini chora kibao.
Alama huwa ni zao,
Lenye manufaa ndio,
Kivuli huishi kwao,
Wapitao na wajao,
Kijana inuka nao,
Lakini chora kibao.
15
Gunia kavu la chumvi,
Hurishai bila chumvi,
Unayengojea mvi,
Kitako kalia jamvi,
Kijana simama nyoka,
Kwa morali na inuka.
Hapana isiyo kapa,
Usubi hutoa lapa,
Kijana huyu kaapa,
Kanuia kuwa papa,
Kijana simama nyoka,
Kwa morali na inuka.
16
Kijana usikimbie,
Hautavaa kiatu,
Kijana na usilie,
Taji hutaona katu,
Kijana vipige vyema,
Vita vyako ujanani,
Kijana ujitambue,
Wewe ni mwana upatu,
Kamba jining'inizie,
Kwa akili ya ubutu,
Kijana vipige vyema,
Vita vyako ujanani.
17
Kijana kushika rungu,
Usitawanye mafungu,
Jifunze kwayo mawingu,
Hayajifungi kwa pingu,
Kijana inuka ndugu,
Na kumrudia Mungu.
Usiiweke mizungu,
Hata sasa nayo tangu,
Usigeuze uchungu,
Kwa utamu wa ukungu,
Kijana inuka ndugu,
Na kumrudia Mungu.
18
Ramani ipo nyikani,
Imeshatupwa jangwani,
Tafakari maishaini,
Ulizaliwa kwanini?
Inuka sasa kijana,
Dhambi nazo kuzikana.
Unafikiri mwishoni,
Ukibweteka mwanzoni,
Maisha yako usoni,
Kwa maono ya yakini,
Inuka sasa kijana,
Dhambi nazo kuzikana.
19
Mwendo sio kuwa mbali,
Ni kuketi kwa halali,
Alivaa kanda mbili,
Na kuchechema mithili,
Kijana usikubali,
Kupumua kwa ajali.
Uliifata asali,
Shari ikiwa dalili,
Jasho la mnyonge kali,
Layanusuu makali,
Kijana usikubali,
Kupumua kwa ajali.
20
Mama aliyekupenda,
Amekwisha kukuzaa,
Hadhi gani unapenda,
Kufa ama kujizaa?
Kijana inuka winda,
Dhahama kila mtaa.
Siku moja wajilinda,
Tamutamu kukataa,
Nafasi ukivurunda,
Ujinga unautwaa,
Kijana inuka winda,
Dhahama kila mtaa.
21
Huwezi kufaidika,
Jasho kutonufaika,
Nini ulichokiweka,
Nyayo zako kuloweka?
Kijana leo chambuka,
Inuka na kamilika.
Mwanzi uliopindika,
Kwao umeshapendeka,
Jema kutopumzika,
Ukiwa waulizika,
Kijana leo chambuka,
Inuka na kamilika.
22
Moja iliyofanyika,
Kileleni yajiweka,
Kijana haujafika,
Cha msingi we inuka,
Andaa mwendo kutoka,
Kesho utanufaika.
Mti uliovunjika,
Shina liliweweseka,
Mizizi yote kung'oka,
Kifo chenyewe chafika,
Andaa mwendo kutoka,
Kesho utanufaika.
23
Kigugumizi ng'amua,
Kutokusita tambua,
Jasho unalohemea,
Chozi unapumlia,
Ujana waelezea,
Amali zisizogoa.
Jimboni uligombea,
Ili ng'ombe kumng'oa
Sifa ukajizolea,
Kumbe unateketea,
Ujana waelezea,
Amali zisizogoa.
24
Gumzo umeshajua,
Kwa kujua kutojua,
Jua linapokuchwea,
Uso wako unawia,
Kijana inuka kua,
Yaliyopita fidia.
Kivuli kilikimbia,
Kwa mwili kunyong'onyea,
Tambua unawezea,
Haifai kuchelea,
Kijana inuka kua,
Yaliyopita fidia.
25
Povu jingi mdomoni,
Umeukosa uoni,
Kula tunda unabuni,
Huu muozo wa mbuni,
Kijana wa duniani,
Inuka twende mbinguni.
Aliishi kwa huzuni,
Kusaliti tamaduni,
Jongoo kafa mtini,
Kinyonga kafa shimoni,
Kijana wa duniani,
Inuka twende mbinguni.
26
Kungwi amechepetuwa,
Kulisimamia buwa,
Hakimu yeye kanawa,
Damu nzito ya mfiwa,
Unga uliopikiwa,
Ujana unakandiwa.
Ni kijana mwenye kuwa,
Alikana kuzaliwa,
Nchi sasa amepewa,
Imani kachokonowa,
Unga uliopikiwa,
Ujana unakandiwa.
27
Vidole huvunja chawa,
Mgonjwa humeza dawa,
Mkomavu ana mbawa,
Mnyonge ye huzagawa,
Kijana si Mwanahawa,
Inuka kanga kunjiwa.
Kijana umeshagawa,
Nguvu zilizozidiwa,
Pembe bovu umepewa,
Kufa nalo wanogewa,
Kijana si Mwanahawa,
Inuka kanga kunjiwa.
28
Ngoja ya mwanahabari,
Ameipinga sheria,
Kwa tundale yu hodari,
Kula kwa kufikiria,
Ujana sio bahari,
Nzi chini katulia.
Aliliunda shauri,
Kwa chozi kujilalia,
Kijana ni mashuhuri,
Mashairi kuyatwia,
Ujana sio bahari,
Nzi chini katulia.
29
Umeukana utumwa,
Kwazo fikra waumwa,
Kifalme umetemwa,
Masikini unagemwa,
Kijana usijepimwa,
Inuka bila kulemwa.
Shambani umeshalimwa,
Mavunoni ukisemwa,
Gudulia limefumwa,
Kitako chako chechemwa,
Kijana usijepimwa,
Inuka bila kulemwa.
30
Usijependa kunyonga,
Shingo uliyoiunga,
Mithili yake karanga,
Mafuta ukayadonga,
Kijana inuka ringa,
Kilichokatika unga.
Kijana wewe machinga,
Hukumu usijepinga,
Ishi kwa ulipo mwanga,
Maisha si kuyatunga,
Kijana inuka ringa,
Kilichokatika unga.