Kijana anayetaka kuikabili hali ya uhaba wa ajira apite hapa

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,345
1,418
Hope wakuu mko fine! Niende kwenye hoja moja kwa moja.

Wakati tukiwa ktk hali tunaposhuudia ongezekezo la idadi ya watu wasio na kazi iwe kwa wasomi na wasioenda shule; vijana bado tunashinda vijiweni ; kwenye social media ku like na kushare; gym eti tunatengeneza body...na mambo mengine kama hayo ambayo hayatusaidii kupambana na changamoto hii ya ukosefu wa ajira na uchumi mbaya.

Wakati hali hiyo ikiendelea wahusika hatutaki kuchukua hatua tukizani kuna mtu mwingine atafanya kwa ajili yetu

Kwa taarifa yako si wabunge wala serikali ya JPM itakayokuja na mwalobaini wa tatizo hili. A matter of fact wewe kuendelea kua jobless ndo fursa kwa wengine kukunyonya na kutajirika.

Nachojaribu kukionyesha hapa ni lazima initiative za kuibadiri hali hii ianze kwa waathirika wa janga hili.

Huu si wakati wa kulialia na kutukana matusi eti hali ni ngumu na waziri kairuki na Simbachawene mbona hawatoi ajira...my frnd utajikuta unaanza kuitwa babu au bibi.

mtaji pekee wa mnyonge ni nguvu zake na maarifa yao. Lazima vijana mthubutu kujaribu yale mnayoyaona hayawezekani

Sina shaka na maarifa mliyonayo hasa kwa wasomi ila nina ukakasi na hali yenu ya kutochukua hatua ktk matendo ili kubadiri hali zenu.

Jengeni na dhibitisheni kuwa ni wenye hali ya kujiletea maendeleo ili kukuza uelewa na kupata uzoefu. Mtaifanikisha dhamira hii kwa kujitolea ( kamwe msikae tu bure...)


Ionyesheni jamii kuwa mnaaminika na mnaweza kuaminiwa ili kuboresha maisha ya jamii ili litawapa nafasi ya watu kuwapa mikopo na mitaji

Onyesheni umoja wenu na nia za dhati kwamba mnaichukia hali hii kwa kuanzisha vikundi vyenye nia ya kufanya shughuri ya maendeleo. Hii itapeleka ujumbe kwa jamii kuwa wapo watu makini wanaopaswa kuungwa mkoni katka juhudi zenu za kunikwamua kiuchumi

Tofauti ya ndoto na kufanikiwa ni kuamua kufanyia kazi kile unachokijua.

Jiamini kuanza. I know its difficult but its not impossible.

Njooni tuchangie ili tusaidiane kutoka .
 
Uhaba gani wakati madaktari wamepata ajira kupitia shinikizo la Kenya
 
Lazima vijana waondoe ile dhana ya kuwaza vikwazo. Ni kama mtoa post umetoa idea nzuri.. lakin baadhi yetu wanapost mshahara mdogo... labda serikal haitatoa mtaji. Vitu kama hivyo...
Vijana wawe na mawazo ya mafanikio.. sio wawaze vikwazo tu muda wote
 
Huu ushauri inaonekana umeuandika wakati umekaa ofisini.......kuna maneno nilitaka niyaweke hapa lakini acha nitunze akiba.
 
Umegusa mkuu mulemule. Ila kuna watu wanareplay sijui ni kutokuelewa, eti madaktari wameajiliwa huyu sijui wa wapi, pamoja na yote mm ni muhanga wa ajira nakupa gwala mzeiyaaaaa
 
Bold,
wacha watengeneze body huoni kila siku casinos na night clubs zafunguliwa
 
Wala hamna haja ya kusema, mazingira tu yatamfosi mtu kupiga kazi na kuzisaka dolari popote zilipo
Mbona Burundi na Uganda wanapiga biashara japo system za serikali zao hazieleweki
 
Mtaji mtaji mtaji ndio shida mkuu....sio kwamba hatuna ideas na nguvukazi..hivyo vipo ila kuupata huo mtaji ndio kazi...Vigezo havikidhi
 
Ulimwengu wa leo huwezi kutoka kama huna capital,njia ambayo kijana anaweza kuitumia kupata mtaji kwa wakati ni kukopa na izo ela za kukopa zina mashart kibao hii inawafanya vijana waogope kwenda kukopa. Ningeomba serilali ndo itoe mikopo tofauti na mashirika Binafsi ambayo ukienda kinyume na mashart wanakufilisi.
 
wakuu kuna fursa kubwa sanaa kwenye mfuko wa vijana wa uwezeshaji chamsingi kuwa kwenye vikundi na kufuatilia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikalini...kukaa kusubiri ufuatwe mlangoni kwako utalalamika sana ..tafakari chukua hatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…