Gulio Tanzania
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,315
- 7,764
Kutokana na hali ya uchumi kuwa mgumu vijana wengi wameangukia kwenye unywaji wa pombe za bei rahisi zinazolewesha haraka kama sungura, master, jogoo nk.
Ukiwa mtumiaji wa hizi pombe huwezi kufanikiwa kimaisha, hizi pombe zinapunguza uwezo wa kufikiria Kuna wengine wanakunywa hizi pombe za kienyeji kama komoni, ulanzi, choya, mnazi hizi ndio usiguse kabisa hata kama umeenda kusalimiwa ndugu zako huko kijijini kwenu usijaribu kugusa pombe hizi.
Sababu gani? Unavyokunywa pombe za kienyeji moja kwa moja unaunganishwa kwenye kufanya ibada za mizimu hivyo kukufunga kabisa kutoka kwenye umasikini.
Tazameni huko mitaani kwenu Hawa watu wanaotumia pombe hizi kama huwa wanabadilika, miaka na miaka wapo vile vile, wanafanya kila kazi lakini hawajawahi kutoboa!
Hata kama unapitia hali ngumu usishawishike kutumia pombe za bei rahisi.