Kifungu hiki cha Katiba hakiendani na wakati

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
949
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
YA MWAKA 1977
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;..

Hiyo sheria hapo juu ya kwenye katiba ilitungwa hivyo tokana
kipindi hicho wasomi wachache, sasa karne hii ya 21 wasomi wengi kuna haja gani ya kuendelea kutumia sheria hiyo?kweli kigezo cha kusoma na kuandika ndio kigezo tosha tu? Angalau mbunge awe na elimu kuanzia degree (shahada) na umri kuanzia miaka 25 miaka 21 ni midogo sana.

Hiyo sheria inapelekea kutupelekea wabunge wabovu bungeni kama wakina Mhe.Joseph Mbilinyi (SUGU) hamna cha maana zaidi ya fujo, hamna sera majimboni wanapita kwa ushabiki.
 
Kila unapofikiria kuhusu katiba na sheria usisahau maadili,mila na desturi za jamii husika tukumbuke tu mfalme Suleman alitoa hukumu ya kesi ngumu kwa maamuzi yenye haki bila ya kuwa na elimu hiyo ya degree lakini maamuzi hayo yanatumiwa mpaka na wenye PHD na hayajawahi kukosolewa. kumbuka tu kuna watu wana busara na hekima kubwa kuliko hao unaosema wanadigirii. Watu wenye digirii mpaka phd mkoani mbeya ni wengi sana lakini fujo za mbeya alizituliza Sugu. siwezi kukulaumu unayo haki ya kutoa maoni
 
Halafu anasema wabunge wengine wanachaguliwa kwa ushabiki tu, sawa..... lakini kuliko kuwaelimisha kwanza hao wabunge bora kuwapa elimu wanaopiga kura kwa ushabiki, wao ndo wana walakin
 
Hivi kativya sugu na aleyesema pawekwe sanamu la diamond nani mtupu?
 
Jamii inahitaji taaluma zote hata wasanii wanastahili heshimu maana mchango wao ni mkubwa katika jamii katika kuelimisha,kuburudisha na kuhudhunisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…