Kifo cha Shetani ndani yetu

Nov 2, 2023
62
66
Mara zote kwenye maisha yetu tumekuwa na dhana ya kusema sijafanya kitu kwa matakwa yangu nimepitiwa au nime shawishiwa na shetani. Neno hilo limetukaa sana akilini na kutufanya kuna muda kujitoa kwenye wajibu wa tulichokitenda na kujutia kujiona hatuja kamilika kuwa wema ndani yetu.

Embu tujiulize kwa makini kwanza? Je, ni kweli toka tupata uelewa kujihusu tumejitambua inavyopaswa au tumeshika mawazo ya tunayo ambiwa tu kwa jinsi watu wengine wanavyo ishi na hatujajitambua kamilifu wenyewe. Kuna mengi tumekuwa tukiambiwa yapo hivi na vile na yakafanya tuyachukue kuwa maisha yetu bila sisi wenyewe kuyachunguza kwa kina.

Turudi kwenye ubinafsi wetu katika matendo yetu ushawishi unatoka wapi. Tunatenda mambo kwa kuyakumbuka, kutamani na mzungoko wa hisia, kushawishiwa au kwa kufikiria ni mema kuyatenda ni wapi msingi wa matendo yetu ulipo. Iwapo tutashindwa kutambua hili tutashindwa kuwajibika na matendo yetu na tutaishia kuwa na dhana ya kufikiri ni shetani anatufanyia uovu ndani.

Embu tuweke tunacho amini pembeni na kuangalia kwa makini zaidi, hisia na mawazo yetu yapo kwenye udhibiti wa ufahamu wetu au ni yanajitegemea kwenye akili kutenda kazi kama uhalisia wako ulivyo. Kuna mambo mangapi akili inayotenda kwa hiari yake mwilini mwetu bila ufahamu wa udhibiti wetu na ni kweli ni matokeo ya mwitikio wa uovu ama ni sisi wenyewe kutojitambua uhalisia wetu uliojificha kwenye uzima wa utendaji wake ndani yetu.

Kwenye maisha yetu tunashawishika sana na maarifa ya nnje yetu lakini tumeshindwa kuwa na muda wa kujitambua uhalisia wetu ndani yetu na kuishia kuwa na akili iliyokuwa nyumba ya mapigano ya hisia na mawazo kushindania matamanio yetu yasiyo na mashiko yoyote kwenye ubinadamu wetu kamili. Muda wote tunakosa utulivu wa akili kujua thamani yetu na nguvu iliyo ndani yetu kwa kuchosha akili yetu wenyewe kwa kuamini mambo mengi yasiyo na uhalisia na kutufanya kupingana na uhalisia ndani yetu na kukosa ubora wetu na ufanisi wa ndani yetu.

Ukweli ni hakuna shetani anaye tupa mawazo na hisia tusizopenda bali ni sisi wenyewe kutojitambua hiari ya akili yetu kuwa na mwitikio kwenye uhalisia wake na kumbu kumbu zake kwa jinsi tulivyo na hakuna tatizo lolote kwenye mwili na akili kutenda hiari zake. Tatizo la kukosa ufahamu wa jinsi tulivyo na kuelewa mwenendo wetu wa ndani kabla ya nnje ndio unatufanya tutengeneze mitazamo mingi isiyo yakweli kujihusu na kutesa maishani mwetu muda wote.

Nb: Ukifikia ufahamu kuwa mwongozo ndani ya akili yako ya hiari iliyo kwenye giza basi akili yako itakuwa na yenye mwangaza isiyo tengeneza tatizo na kuwa na utulivu wenye amani utaoleta matendo yasiyo na majuto wala pingamizi ndani yetu.
 
Back
Top Bottom