OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,092
- 114,645
Mchezaji wa Simba aliyefunga bao pekee katika mechi ya jana akiifungia timu yake ya Simba dhidi ya wenyeji Mbeya City ametolea ufafanuzi goli alilofunga jana
Goli hilo limezua mjadala katika mitandao ya kijamii baada ya uongozi na mashabiki wa Yanga kutuhumu kwamba mfungaji aliotea
Kichuya ambaye amekuwa akiifunga Yanga katika mechi tano mfululizo amesema kuwa refa alijiridhisha kuwa hakuotea
Akizungumza na Azam TV mara baada ya mchezo anasema aliwazunguka mabeki wa Mbeya City kwa mbele huku wao wakibaki kumtazama tu. Amefafanua kuwa kama angewazunguka mabeki kwa nyuma ilikuwa ni off-side dhahiri lakini trick aliyoifanya iliwachanganya mabeki
Anasema angeshangaa kama refa angekataa goli lake
Golikipa wa Mbeya City aliweka wazi kuwa Simba ni timu kubwa nchi hii ni lazima iheshimiwe