Kibu kuisumbua Simba, Taswira mbaya kwa timu

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
938
1,654
Moja ya nguvu kubwa ya binadamu aliyopewa ni uwezo wa kufanya chaguo(Choices). Japo knowledge yangu bado ni limited, ili sina imani kama hata malaika wamepewa nguvu ya kufanya machaguo kama alivyopewa mwanadamu. Unaweza kuamua hata sasa kufanya mabaya au mema, kujenga au kubomoa, kuishi au kutoa uhai, e.t.c

Wengi tunaamini mwanadamu ni intelligible and reasonable being, wakimaanisha kuwa anaweza fanya right choices bila influence yeyote. Kufupisha maada ngoja niende moja kwa moja ya kuwa anafanya binadamu tunafanya mema, mazuri sababu ya faida zinazopatikana kutoka kutokana na matendo hayo. Inaweza ikawa ni kweli. Lakini wapo wanafanya hivyo kwa kuogopa matokeo yakushindwa kutofanya hayo mema.

Bila tishio la jehanamu(Hell) sidhani kama binadamu wangekuwa wema namna hii. Bila kuambiwa waovu watachomwa moto hii dunia ingewa tayari tumeiangamiza. Bila sheria za adhabu na katazo mambo ni ovyo ovyo. Angalia wakati wa Magufuli na Mama baadhi viongozi ni wale wale, ila angalia kinachofanyika sasa ni mbingu na ardhi. Hofu ndio kitu pekee chenye uhakika wakum-shape mtu endapo akili binafsi imeshindwa.

Angalia katika ngazi ya familia-watoto hawarudi nyumbani sababu ya usalama wao ai itawasaidia wao kupata muda wa kupumzika, ila wanarudi sababu wanajua nikichelewa kurudi nyumbani lazima moto uwake, shuleni, e.t.c. Mpe mtoto uhuru bila mipaka(vitisho) majibu utayapata.

Mzee wangu alishawahi niambia kuwa hofu ni kitu pekee kinaweza fanya hata kile kitu ambacho hakina uwezo kwa kufikiri kikatii. Angalia Mbwa, Paka ukimkataza jambo fulani, badae akapata adhabu, aah haji kutenda tena lile kosa. Fear. Mkamate kijana muulize unataka mpenzi wa namna gani “ Mwenye HOFU ya Mungu itakuwa moja ya sababu kubwa”.

Turudi kwa Simba, kwanini alivyoondoka tu mzee wetu Hans Pope, kila kitu kilibadilika. Kwani aliondoka na akili za wachezaji au viongozi wetu? Alivyokuja kuondoka Barbara ndio kabisa. Tunakubali tumesumbuliwa sana na Chama. Ila mchezaji aina ya Israel anaiambia Club kuwa kama mnataka mimi nibaki, basi kapombe atoke. Labda kweli kuna mambo behind lakini hii nguvu wanaitoa wapi? Hii nguvu ya kuchezea P*mbu za nyati wanaitoa wapi?

Leo ni story ya kibu. Kuhusu Kibu naomba niishie hapa. Ila Simba jaribuni kutengeneza mstari, rudisheni standard yenu. Nyie si ndio mlikuwa mnafuatilia sio tabia tu, bali hata usafi wa mchezaji. Vijana walikuwa wanapendeza. Mmekata Rasta chafu chafu nyingi sana. Leo timu ni kama Migos. Nyie si ndio mlikuwa mnauwezo hata wa kupeleka vijana kupima akili zao, au matumizi ya madawa? Haya mambo yameishia wapi?

Fuatilieni hili. Ikishindikana kuheshimiwa atleast basi vijana waogope. Lakini nje ya hapo tutaendelea kutengeneza bomu kila kukicha. Huyu tu-sacrifice ili iwe mfano kwa akina Kibu wengine.

Edit: Asante sana Klabu ya Simba kwa kusimamia hili. Naomba huyu awe mfano kwa wengine.
 

Attachments

  • GTL_2STWoAEFLKy.jpeg
    GTL_2STWoAEFLKy.jpeg
    1.2 MB · Views: 4
Wamuache akapauke..cha kufanya ashtakiwe na alipe hiyo hela ya mnyama...then aendelee na wazungu wake
Mkuu hakuna usumbufu wowote., kwani kibu keshasaini Simba na kulipwa kisha akatoroka?

Kibu yupo huru kuamua analoamua, kama kahitaji muda zaidi kutafakari hatma yake ni sahihi kabisa, binafsi naona yeye ndo anasumbuka iwapo hajajua anataka nini, Simba haiwezi kosa mbadala wake.
 
Mkuu hakuna usumbufu wowote., kwani kibu keshasaini Simba na kulipwa kisha akatoroka?
Kibu yupo huru kuamua analoamua, kama kahitaji muda zaidi kutafakari hatma yake ni sahihi kabisa, binafsi naona yeye ndo anasumbuka iwapo hajajua anataka nini, Simba haiwezi kosa mbadala wake.
Kumbe hajasaini..ndo maana sijamuona kwa wale waliotambulishwa...
 
Kumbe hajasaini..ndo maana sijamuona kwa wale waliotambulishwa...
Ninavyofahamu bado hajasaini na huenda hajasema kama atabaki Simba au ataenda pengine. Huko kutokusema kwake ndo kunawaweka mashabiki kama huyu njia panda sababu hawajui Kibu ni mchezaji wa Simba au la. Soka ni maslahi.
 
Mkuu hakuna usumbufu wowote., kwani kibu keshasaini Simba na kulipwa kisha akatoroka?
Kibu yupo huru kuamua analoamua, kama kahitaji muda zaidi kutafakari hatma yake ni sahihi kabisa, binafsi naona yeye ndo anasumbuka iwapo hajajua anataka nini, Simba haiwezi kosa mbadala wake.
Kwa kweli Kibu siyo aina ya mchezaji wa kuisumbua Simba,mshambukiaji msimu mzima kafunga kagoli kamoja sasa wa nini huyu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom