ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 146
- 166
MAMA NDIO CHANZO CHA WIMBO WANGU ( KIBANDA CHA SIMU )BY SOGGY DOGGY
Soggy Doggy amesema chanzo cha yeye kuandika wimbo huo ni baada ya mama yake kupenda kufungia simu yao ya mezani ili kuogopa bili kuwa kubwa kwa watu kupiga hovyo, na kusababisha awe anakwenda kupiga simu kwenye vibanda vya simu, ambavyo kwa miaka hiyo vilikuwa kila kona ya mtaa.
"Kibanda cha simu ilianzia tuseme ni home, kwa sababu simu iliyokuwepo ilikuwa ni simu ya mezani, lakini mama muda wote ile simu, unajua simu za zamani zilikuwa zinapigwa kufuli pale, yani huruhusiwi kwenda kujipigia pigia tu masimu kwa sababu bili ikija itakuwa ni kubwa, kwa hiyo alichokifanya mama alikuwa anaifunga ile simu huwezi ukaenda tu mtu ukajipigia, kwa hiyo muda mwingi ilikuwa mi nikitaka kupiga simu ilikuwa inanilazimu niende kwenye vibanda nikapige simu, so nikiwa katika hivyo vibanda kupiga piga simu, nilikuwa naona ona hivyo vituko, yani huyu kaja amefanya hiki amefanya vile, so nikaamua kujiongeza kwenye kuandika, alafu nilikuwa naandika kama ni wimbo wa masihara", alisimulia Soggy Doggy juu ya stori ya kibanda cha simu.
Soggy aliendelea kusema kuwa wimbo huo alitakiwa kushirikiana mwanamuziki wa kike ambaye kwa wakati huo alikuwa anafanya poa kwenye game ya Bongo Fleva, Rema Chalamila au Ray C, lakini alimtosa na ndipo akafanya na Josephine.
"Namshukuru Majani, Josephine aliyeshiriki, kwa sababu wimbo pia ulikuwa ni Ray C alitakiwa ashiriki, lakini Ray C hakujisikia ama aliona Soggy wa nini mimi, japokuwa Soggy ni kaka yake kwa mbali tu, ye akachukulia wa nini akakimbia kimbia, nashukuru Josephine nilimkuta studio hapo hapo, akashiriki kwenye wimbo na wimbo ukahit", alisema Soggy Doggy.
Msanii wa bongo fleva ambaye bado yupo kwenye game, Soggy Doggy, ametoa siri ya wimbo wake wa 'kibanda cha simu' ambao ulifanya poa sana miaka ya 2000, na kilichompelekea yeye kuandika wimbo huo ambao hauchuji masikioni mwa watu kwa ujumbe wake.
SOGGY- KIBANDA CHA SIMU
Nje ya kibanda Cha simu tangazo la uzushi
Mkopo umesafiri kinachotakiwa keshi
Ni mia tano kila dakika utayoenda hewani
Kubeep sh' hamsini sipigishi za mezani
Haya sasa mteja twende ndani ya kibanda
Machache poa mengi yanayotokea sijayapenda
Wateja wangu wengi tabia zao huwa chafu
Matusi kejeli ugomvi sio waaminifu
Kuna mteja wangu mmoja jina lake nanii
Jina lake siwatajii asije kuninanii
Kila akija kupiga simu yeye huwa bwii
Mambo yake hadharani sababu ya bwii
Si kama mteja wangu mmoja jina lake Achebe
Kila akija kupiga simu ye analeta ubabe
Yani anapiga zaidi ya tano
Lakini nashangaa hanipi hata senti tano
Wateja wanaonipa raha mmoja wapo Chesco
Kila akija kupiga simu mi' napata vicheko
Mkononi ana tunda na lugha yake sijui Kindengereko
Mara ainame mara asimame ilimradi vituko
Presha inapanda wakija wateja Wahaya
Wanaodhani labda Soggy mi' sio Muhaya
Mara utawasikia(native language)
Hicho kibanda Cha simu
Kinachompa Soggy wazimu
Hicho kibanda Cha simu
Lakini kwake ye' muhimu
Japo napata pesa lakini napata presha
Wateja utulivu zero kifupi wananidatisha
Najua mambo mengi sababu ya kibanda cha simu
Najua ni watu wangapi Mr Chance kashawadhulumu
Pata picha mteja Salim Chumu
Kila anapokuja huwa nataka kubwia sumu
Kila namba anayopiga nahisi kizunguzungu
Kama sio ya dada yangu utakuta ya demu wangu
Najifanya fala kisa nafanya biashara
Nikisema nisimpigie basi si ntakosa hela
Kusema kweli inahitaji uvumilivu
Nashangaa sizili mbivu nachopata maumivu
Marafiki nao kibanda changu ndo maskani
Ni mimoshi ya sigara asubuhi mpaka jioni
Yote tisa siku sitosahau
Siku hiyo bado kidogo Soggy mi' nishikwe wehu
Alitokea mwarabu mwenye ndevu kama za Osama
Akataka nimpigie nisipopiga itakuwa noma
Aliongea Kiarabu nisielewe anachosema
Katikati ya maongezi eeh si akaitaja Dodoma
Wakati anaendelea akamtaja Spika Bunge
Maswali nikajiuliza anataka kulipua Bunge
Akanipa elfu kumi hata chenji hakumbuki
Aliondoka harakaharaka si alikuja na pikipiki."
#funguka
.
UKWAJU WA KITAMBO
0767 542 202