Kesi ya waliotumwa na afande kubaka na kulawiti yaendelea leo

jjackline

Senior Member
Jul 25, 2024
111
273
Kesi ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, inayowakabili washtakiwa ‘wanaodaiwa kutumwa na afande’ leo Jumatatu, Septemba 2, 2024 inaendelea kusikilizwa.

Wakili anayewawakilisha washtakiwa, Godfrey Wasonga amesema kuwa kesi hiyo itasikilizwa mfululizo kuanzia leo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas, maarufu kama Nyundo, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Soma Pia: Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Zabibu Mpangule. Walikana mashtaka hayo.

Snapinsta.app_457725548_1721426478626626_3537230210117422140_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom