Kesi ya uamsho huenda ikafutwa hivi karibuni

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
792
1,144
+259 [HASHTAG]#Zanzibar[/HASHTAG]

Na: Salma Said

MAHAKAMANI VUGA:Kesi ya Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) huenda ikafutwa hivi karibuni kufuatia upande wa Serikali kushindwa kuwaleta Mahakamani hapo watuhumiwa hao wanaokabiliwa na kosa la uvunjifu wa amani, uharibifu wa mali za Serikali na kuzusha taharuki nchini.

Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wameahidi kuwaleta Mahakamani hapo na iwako wakishindwa wataiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo.

Jaji anayeisikiliza kesi hiyo Fatma Mahmoud ambaye kipindi kilichopita alitishia kujitoa kusikiliza kesi hiyo, amekubaliana na upande wa DPP na ameiakhirisha kesi hiyo hadi tarehe 13.6.2017. (ALLAH ajaalie wawe huru na wakajumuike na familia zao kwenye Ramadhan hii. Ameen).

In sha ALLAH tuzidisheni dua kwa ndugu zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…