Kesi ya Mbowe: Mashahidi wa Mashtaka wana nini Kipya?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
31,622
41,657
Kwa hakika tangu kesi nzito hii kwa jina imeanza, ushahidi wa kuendana nayo umeshindikana kutolewa.

Bila shaka kwa upande wa mashtaka, ushahidi wa Luteni Urio ulikuwa ndiyo wa muhimu zaidi.

Lakini kama ni hawa kina Mahita, Kaaya, Wauza mbege, Kingai au yule jamaa wa Tigo, labda ilikuwa muda sasa kwa upande wa mashtaka kuanza kujipanga kufunga tu sehemu yao ya ushahidi.

Ukimwangalia shahidi wa jana #7, bwana Mahita Omary Mahita akitokea kwa mara ya pili mahakamani, inafikirisha:

1. Wakati kwenye shauri ndani ya shauri Mahita alikanusha yeye kuwa mwanasheria, jana alithibitisha kuwa yeye kumbe ni mwanasheria.

Jana:

IMG_20211106_122207_157.jpg


Sept 17:

IMG_20211106_124948_999.jpg

Updates: Yanayojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi

2. Wakati kwenye trial within trial alidai Adamoo alikamatwa na Bastola Luvern A5340, jana alisema Bastola ilikuwa Luger A5340.

Jana:

IMG_20211106_122104_267.jpg


Sept 17:

IMG_20211106_133008_668.jpg


3. Wakati mapema alisema kwenye ukamataji walikuwa polisi sita, alibadili kuwa tano, sita na hata tano tena kabla ya kuhitimisha kuwa hakuwa ameeleza kabisa:

IMG_20211106_135713_518.jpg


IMG_20211106_135805_858.jpg


Yanini kuendelea na mashahidi wa namna hii? Mbona upo mwendelezo wa wazi tu kuwa:

A: Maamuzi kuhusiana na hoja zote zisizoathiri hukumu ya mwisho ya shauri la msingi, uzoefu unaonyesha zinatolewa in favor ya upande wa utetezi?

B: Maamuzi kuhusiana na hoja zote zinazoathiri hukumu ya mwisho
ya shauri la msingi, uzoefu umeonyesha zinatolewa in favor ya upande wa mashtaka?

Kesi ya Mbowe: Ushahidi upande wa Mashtaka unapochukuliwa kuwa ndiyo Dhahiri

Ushauri wa bure kwenu Mashtaka:

"fungeni tu sehemu yenu ya ushahidi hakuna jipya. Mizani iko upande wenu."
 
Hadi sasa sijaona ushahidi wa kuwafanya hawa washitakiwa kuwa magaidi.....plans zao ...vilipuzi etc...mabomu mpango mkakati ukoje watalipuaje ......mabomu wanapata wapi waliingizaje nani anawaletea kuwauzia..etc la sivyo kuchafua nchi tuhuma za kitoto magaidi wako msumbiji huko huyo kingai na mrembo mahita waende huko ndio wataekewa uouuzi wao wa kuchezea kodi hatutaki nyambafuu kbss
 
kipya kipo. Shahidi ameshindwa kueleza namna gani Mbowe alikuwa anaratibu ugaidi vividly. Ye anasema alikuwa anaratibu tu. Majina ya sheli zilizopangwa kulipuliwa hawajui

Haupo ushahidi wenye kueleza hayo lakini hukumu ya shauri ipo na haibadiliki.

Mwendelezo umekuwa wazi:

A: Maamuzi kuhusiana na hoja zote zisizoathiri hukumu ya mwisho ya shauri la msingi, zinatolewa in favor ya upande wa utetezi.

B: Maamuzi kuhusiana na hoja zote zinazoathiri hukumu ya mwisho
ya shauri la msingi, zinatolewa in favor ya upande wa mashtaka.

Yanini kuendelea na mashahidi wanaokuja hata kukoroga mambo kama bwana Mahita wakati hukumu ipo tayari?
 
Kipya kwa mashahidi ni tamaa yawao kupewa mamlaka ya kuwa watoa hukumu🏃.

Tamaa yao hiyo haina tija kwao kwa sababu mashahidi wao sana sana wanazidi kujichanganya wakati hukumu imekuwapo tayari.
 
Back
Top Bottom