Kesi ya Mbowe: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi atajwa kumtumia pesa Mtuhumiwa

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,901
92,509
Hii kesi itavua Watu nguo saana, nakiri nilikua sahihi kusali usiku na mchana isifutwe.

Muda huu kwenye cross examination, Mtobesya anamtaja Aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi Ndugu Mwinyi kuwa alimtumia pesa Mtuhumiwa ndugu Bwire.

Judge kaona isiwe tabu, kauliza kama wako tayari Waziri huyo aitwe, wakajibu NDIO MUDA UKIFIKA.

--
Mallya: Sasa Kwenye Miamala ya Khalfani Bwire, Ina onyesha alikuwa anatumiwa Fedha na Waziri wa Ulinzi Kipindi Kile Ambaye ni Hussein Mwinyi ambaye sasa ni Rais wa Zanzibar, Ila Wewe Ukaona Ufiche tusione Miamala hiyo.

Jaji: Bwana Mallya, Unatoa wapi Maelezo hayo?

Malya: Kwa wateja wetu Jaji


 
Hii kesi inavyokwenda Mawakili wa utetezi wanataka kueleza Kila Jambo lililofanyika sirini na kuwataja wahusika. Lakini pia ulimwengu ulivyo Sasa hakuna binadamu wakumwamini. Taarifa nyingine zinatoka Kwa watu waliopewa Madaraka lakini wana hofu ya MUNGU.

Nikiangalia namna Kigogo 2014 anavyopost Leo najiuliza access ya taarifa imekatikaje Baada ya JPM tu kuondoka? Je, palipokuwa panavuja palizibwa vipi mapema hivyo?

Kwa mfano huu ndipo ninapoamini ukitenda Haki utaheshimika na kulindwa, ukiwakosea watu ambao wanakwenda nyumba za ibada kutubu unazalisha watu ambao toba sahihi nikufichua Yale maovu yanayoendelea yasiendelee au jamii ipige kelele usiendelee kuyafanya

Naomba Serikali iangalie kinachoendelea mahakamani kama kina tija Kwa ustawi wa Serikali na nchi kwa ujumla.

Marais wawili kutajwa kwenye cross examination siyo Jambo dog hata kidogo,
 
Back
Top Bottom