Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,463
Na. Sheikh Ponda Issa Ponda
Kesi iliyofunguliwa na Waumini wa Kiislamu 12, dhidi ya MSAJILI WA VYAMA VYA KIJAMII WIZARA YA MAMBO YA NDANI, Kabidhi Wasii (RITA), MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, BAKWATA na BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU hivi karibuni imetajwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Kirekiano.
Waliohudhuria ni wadai pamoja na mawakili wao ambapo kwa leo walikuwepo watatu, Wasomi Juma Nassoro, Yahya Njama na Ubaid Hamidu.
Upande wa Serikali waliwakilishwa na Wakili wa Serikali Edwin Wibiro.
BAKWATA waliwakilishwa na Wakili Rafii Fatihu.
Ambapo BARAZA KUU waliwakilishwa na Wakili Buruhani Mussa.
Wakili wa serikali aliitaarifu Mahakama kuwa wameshajibu madai ya wadai na wameweka mapingamizi. Vivo hivyo wakili wa BAKWATA aliitarifu Mahakama kuwa wameshajibu na wao pia wameweka mapingamizi.
Kwa upande wa BARAZA KUU wakili wao alichelewa kufika mahakamani lakini Katibu Mkuu Ramadhani Seif aliitaarifu mahakama kuwa na wao pia wameshajibu. Hata hivyo alisema hakuwa na maelezo ya ziada kwani taarifa kamili alikuwa nayo wakili wao ambaye alichelewa kufika mahakamani.
Baada ya mahojiano mafupi kati ya mheshimiwa Jaji na mawakili wa pande zote walikubaliana kuwa kesi iahirishwe ili kutoa nafasi kwa wakili wa BARAZA KUU aje kutoa ufafanuzi wa majibu ambayo mteja wake alijibu.
Aidhai pamoja na hayo kuna mambo ya kisheria ambayo mawakili wanapaswa kuyafanyia kazi ili watakapokuja tarehe inayofuata waweze kuifafanulia mahakama nini cha kufanya ili shauri hilo limalizwe katika hatua ya awali ndani ya muda wa kisheria ambao ni siku 30.
Baada ya atua hizo shauri limeahirishwa mpaka tarehe 10.12.2024 saa 2 kamili asubuhi.
Msingi wa kesi
Shauri hili dhidi ya serikali na BAKWATA imefunguliwa na watu mashuhuri 12 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara:
1. Sheikh Ayoub Salim Muinge (Morogoro)
2. Sheikh Prof. Hamza Mustafa Njozi (Morogoro)
3. Sheikh Ponda Issa Ponda (Dar es Salaam)
4. Ustadhi Bakari Bakari Shingo (Dar es Salaam)
5. Bi. Riziki Shahari Mngwali (Dar es Salaam)
6. Ustadhi Juma Husein Kilaghai (Dar es Salaam)
7. Ustadi Abdallah Mohammed Saidi (Dar es Salaam)
8. Ustadhi Twalib Muhammad Twalib (Dodoma)
9. Ustadhi Ibrahim Hussein Sherally (Mwanza)
10. Ustadhi Mussa Rafiki Marua (Dar es Salaam)
11. Ustadhi Abubakar Ibrahim Mngodo (Dar es Salaam)
12. Ustadhi Mustafa Mohammed Abeid (Dar es Salaam)
Viongozi hao kwa niaba ya umma wa Kiislamu wanapinga kitendo cha serikali kuweka sharti kuwa hakutakuwa na Jumuiya au Taasisi au Msikiti utakaopewa sehemu ya haki za msingi (kama kusajiliwa RITA au WIZARA YA MAMBO YA NDANI bila kwanza kuridhiwa au kupata barua ya utambulisho kutoka BAKWATA). Kitendo hicho ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara.
BAKWATA na BARAZA KUU wamejumuishwa katika shauri hili kwa misingi ya kisheria lakini kwa hakika waliofungua shauri wanailalamikia Serikali kwa kuvunja katiba ya nchi kuwalazimisha waumini wote wa dini ya kiislamu pamoja na Misikiti yao, Jumuiya zao, Taasisi zao nyingine kama hizo kuwa chini ya BAKWATA.
Amri au hukumu ya Mahakama inayoombwa ni mwisho wa kesi mahakama kutamka na kufuta ulazima wa Misikiti, Jumuiya, Taasisi na Waislamu kwa ujumla kufanywa kuwa ni wafuasi wa BAKWATA bila ridhaa yao.
Waliofungua kesi hawana makusudio yoyote ya kuwalazimisha wale wote ambao ni wafuasi wa BAKWATA ikiwemo misikiti inayomilikiwa na BAKWATA kwa kujenga au kupewa isiwe chini ya taasisi hiyo. Kinachopingwa ni kulazimishwa kwa waumini wote wa dini ya kiislamu na taasisi zao kuwa chini ya udhibiti wa BAKWATA bila ya ridhaa yao.
Waliofungua shauri wanakusudia waumini wa Kiislamu watakapotaka kusajili taasisi yao jumuiya yao au msikiti wao waachwe huru kuamua ni taasisi ipi waipendayo kuwa taasisi kuu kwao (supreme authority).
Wamefungua shauri hili wakiwa na uhakika hiyo ndivyo katiba ya nchi inavyotaka na hata sheria zinavyotaka kinyume na msimamo wa Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani na RITA wanavyolazimisha.
Pia, soma: BAKWATA yafunguliwa kesi, kisa na mkasa Mamlaka yake ya kidini