Pre GE2025 Kesho Utafanyika Upasuaji Mkubwa kwa wagonjwa CHADEMA, Madaktari 1,200 kuendesha zoezi hilo. Je, mgonjwa atatoboa au atakata moto?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
28,176
67,726
Hayawihayawi!

Kesho tarehe 21 itafanyika Operation kubwa kwa mgonjwa ambaye hapa ni CHADEMA.

Madaktari wasiopungua 1200 wataendesha zoezi hilo. Kiukweli mgonjwa yupo taabani. Upasuaji huu ni muhimu Sana lakini pia ni Upasuaji Hatari kama madaktari hao hawatakuwa Makini kufanya zoezi Hilo.

PATIENT HISTORY

1. Mgonjwa yadaiwa ugonjwa wake ulianza mwaka 2015.

2. Yapo madai mawili kuhusu chanzo cha ugonjwa wake;
a) Mgonjwa alipewa Sumu
b) Mgonjwa alipandikiziwa Vimelea (virus) hatari vya kuharibu Ubongo na Moyo wake.

3. Ugonjwa ulianza kuchachamaa zaidi Miaka ya 2018

4. Mwaka 2022 Seli kuu ya kulinda mwili wa Mgonjwa ilipatwa na shambulizi Hatari na kujikuta limezingizwa na Vimelea Hatari. Hali iliyopelea Seli hiyo kuu ya kinga kupoteza ufanisi katika kufanya Kazi kuu ya kuongoza majeshi ya kulinda Mwili wa Mgonjwa.

5. Mwaka 2023 Mwanzoni Seli kuu haikuwa na uwezo wowote tena. Ilishaharibiwa na sasa ikawa inadhuru mwili wa Mgonjwa.

6. Mwaka 2024 Seli zingine za Mwili zikaanzisha harakati kunusura afya ya Mgonjwa. Hivyo Njia pekee ni kuondoa Seli kuu.

7. Mwaka huohuo Seli kuu saidizi ikatangaza kuchukua nafasi ya Seli Kuu. Hii ikafanya Ugonjwa kuchachamaa. Hali iliyopelekea Mgonjwa apelekwe Hospital na kupewa Rufaa apelekwe hospital kubwa Kabisa ya taifa. Huko kuna madaktari wa kuhangaika na ugonjwa huo.

8. Madai ya Seli ambazo hazitaki kuongozwa na Seli kuu yanasema, Seli kuu imedukuliwa na kuharibiwa vibaya kwenye mfumo wa Neva na Mifumo ya mzunguko wa damu. Hii inafanya Vimelea na virusi kumtumia Seli kuu kuushambulia mwili wa Mgonjwa

Hii ni kusema, Mgonjwa ambaye ni CHADEMA anasumbuliwa na matatizo mawili,
Moja, Vimelea Hatari kuingia Ubongoni.
Pili, Vimelea Hatari kushambulia mishipa ya Moyo.

Hivyo Kesho Upasuaji utakaofanyika ni wa Ubongo na Moyo. Hii inafanya Upasuaji huu kuwa Mkubwa zaidi Duniani kufanyika kwa siku Moja. Hii itapelekea madaktari wasiopungua 1200 kuendesha zoezi Hilo.

Wapenzi, ndugu, jamaa wa Mgonjwa CHADEMA wanawasiwasi Mkubwa kuhusu zoezi Hilo
Kwani Seli kuu yenyewe imegoma kuondolewa kwa ajili ya manufaa ya Mgonjwa.

Kesho ni Do or Die
CHADEMA inaenda kufa au kuzaliwa upya.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom