Kesho nampeleka mwenza wangu Clinic, vitu gani vya kuzingatia?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,941
24,816
Niko na mwenza naishi nae, bado sijaoa ila niko nae tu kuvukisha kipindi hiki cha baridi kipite salama bila kubanwa na Ngiri. Mwenza wangu ni mjamzito, na kesho namsindkiza clinic kwenda kumfungulia kadi.

Kwa kweli sijawahi kwenda huko, watoto wangu wote ni mama zao tu ndio walikuwa wanaenda. Je, vitu gani vya kuzingatia nikiwa Clinic, maswali na nk? Bila kusahau muda sahihi wa kufika kutuo cha afya.

Wasalaam soon nitachange ID from zero IQ to baba fulani.

1628695095933.png


Cc Zero IQ

Pia soma: Mrejesho baada ya kumpeleka mwenza wangu Clinic
 
Uliza kuhusu afya ya mzazi mwenzio kulingana na vipimo mtakavyofanya.

Waambie wakufundishe namna ya kutathmini kile kitakachoandikwa kwenye kadi na uliza kuhusu lishe ya mgonjwa, I mean anatakiwa kula vyakula gani kwa ajili yake na mtoto.

Anza na hivyo
 
Baada ya hapo usisahau kuwa unarudi na mzazi mwenzio kila tarehe ya clinic ikifika, maana wanaume wengi tuna kasumba ya kuingia mitini siku ya clinic.
 
Back
Top Bottom