Kero zangu kwa CRDB wakala

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,853
15,846
Nimefanya huduma ya uwakala wa CRDB kwa takribani miezi 8 sasa na hizi ndio kero zangu;

Kero nyingi ziko based na ubovu wa mtandao/Customer Care

Sijajua kama tatizo ni hizi machine mpya tulizopewa ama ni tatizo la machine zote (POS), maana kipindi naanza niliwekewa chip ya Airtel, kero ya mtandao ilikuwa ni kubwa sana japo niko ndani ya eneo ya manispaa (mjini), yaani kwa mfano umepata wateja 50 kwa siku basi wateja 25 unaweza ukashindwa kuwahudumia kwa sababu ya kufeli kwa mtandao, na mtandao unafeli mara kwa mara kwenye malipo ya bill hasa luku, ikifuatiwa na ving'amuzi, baada ya kero hii kuonekana kubwa nikaenda ofisini kwao na kuomba kama kuna uwezekano wanibadilishie chip, na kweli wakanibadilishia wakanipa Voda lakini bado kero haikwisha japo ilipungua kidogo.


Baada ya status kuwa failed na balance kupungua unaamua kuwapigia ili ujue tatizo; bahati mbaya customer care kuwapata inaweza kukuchukua dakika 15 hadi nusu saa, wakati huo unahitajika kuwahudumia wateja wengine (na kumbuka asilimia kubwa ya wanaoendesha huduma hizi wanakuwa na biashara nyingine pia).

Sasa kwa mfano muhudumu wakati huo uko peke yako, na uko na wateja wengi huwezi ukaanza kuwapigia huduma kwa wateja ambao wanapokea baada ya dakika 15-30 huku wateja wengine wanasubiria huduma, wakati mwingine unalazimika kumrudishia pesa mteja ukiamini muamala umefeli, sasa ukitulia ukaamua kuwapigia ccare ndo unapochoka, watakwambia huu muamala umefanikiwa ila bahati mbaya token zilishindwa kuwa processed hivyo tunakutumia token ya mteja kwa njia ya sms
, kumbuka hapo mteja pesa umeshamrudishia na kaenda kununua luku kwingine na pengine huyo mteja humfahamu. Kwahiyo hapo moja kwa moja unahesabu LOSS.




NB: Kuna kero nyingi nimekutana nazo kwenye huduma ya CRDB Wakala hapo nimeelezea chache tu kama mfano, mimi sio mgeni kwenye hizi huduma za kifedha hivyo hadi nimeamua kuandika hivi ujue nimekutana na kero za kutosha na nnaamini CRDB wanapitia pia JF, watatafuta namna wa kurekebisha haya.

Niwapongeze mitandao ya simu naona wao wameendelea kidogo hasa upande wa Customer Care/ Ubora wa Mtandao kwa mijini/ na Usalama wa pesa wa wakala. CRDB wana mengi ya kujifunza, yaani viloss loss vya ajabuajabu kwa CRDB imekuwa kawaida, tofauti na mitandao ya simu ambayo viloss inakuwa ni uzembe wako mwenyewe wakala.

NAWASILISHA.
 
Daaaa...machine za crdb zinasumbua sana hasa upande wa luku na kulipia visumbuzi.
 
Daaaa...machine za crdb zinasumbua sana hasa upande wa luku na kulipia visumbuzi.
Vipi Azam Pesa una experience nayo? Nafikiria kuitafuta kama iko vizuri ili mambo ya kulipia bill nitumie hiyo, huku kwenye pos ya crdb ibakie kuweka na kutoa tu
 
Nenda branch omba wakupe card kwa sasa zinatolewa baada ya malalamiko mengi ya mawakala network, kabla mteja hajaondoka angalia statment na mteja wa luku usirudishe hela asubiri token atatumiwa
 
Vipi Azam Pesa una experience nayo? Nafikiria kuitafuta kama iko vizuri ili mambo ya kulipia bill nitumie hiyo, huku kwenye pos ya crdb ibakie kuweka na kutoa tu
Hapana.na sizan kama wana machine
 
Nenda branch omba wakupe card kwa sasa zinatolewa baada ya malalamiko mengi ya mawakala network, kabla mteja hajaondoka angalia statment na mteja wa luku usirudishe hela asubiri token atatumiwa
Sorry, hiyo kadi inasaidia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…