Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Aeronautical

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
206
344
Habari za jioni ndugu,

Kwa sasa maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam hasa maeneo ya Manzese napoishi kumekuwa na kero kubwa ya maji na maji yanaweza kutoka lisaa limoja tena mara moja kwa mwezi mzima.

Na DAWASA wamekaa kimya hakuna wanachoeleza cha maana ukiwapigia simu. Ni vyema sasa Waziri wa Maji na DAWASA kwa ujumla watangaze rasmi mgao wa maji na kutupa ahadi ya kufanikisha upatikanaji wa maji kama walivofanya TANESCO kipindi cha mgao wa umeme.

Niwapongeze TANESCO kwakweli siku hizi huduma ya umeme imetengemaa na sasa DAWASA kuna shida kubwa ambayo wanasiasa wamekaa kimya na magazeti nayo wamejifanya wapo kimya ila wananchi wengi sana wanaumia.

PIA SOMA
- KERO - Waziri Juma Aweso atoke hadharani na kusema kwanini Ubungo mpaka Kimara maji ni shida

- KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

- Maji Dar ni Shida isiyomithilika wakati Mto Ruvu umejaa!
 
Hao TANESCO usiwataje taje awachelewi kukianzisha.

DAWASA wanazingua sana. Na kama unakaa Kimara ukijumlisha na utanuzi wa barabara wanakata sana mabomba ya kusupply maji.
 
Hao TANESCO usiwataje taje awachelewi kukianzisha.

DAWASA wanazingua sana. Na kama unakaa Kimara ukijumlisha na utanuzi wa barabara wanakata sana mabomba ya kusupply maji.
TANESCO kwa kweli safari hii wanafanya kazi nzuri sana kwa mie napoishi na nawapongeza kwa sasa ila DAWASA kwakweli inabidi watupe taarifa tujue shida ni nini hasa na watangaze mgao na sio kukaa kimya.
 
Dawasa ni kero yaan maji hamna miez minne sasa wanajibu simple tu sasa wanafanya biashara gani.
 
Kuhusu umeme ,Samia apongezwe kwakweli, naambiwa na suala la maji inakoendea mgao itakua historia
 
Na wamekaa kimya ata vyombo vya habari na kumsifia tu Aweso wakati anachokifanya hakuna. Wajifunze kwa TANESCO hivi sasa.
Yan shida. Pamoja na mvua zote sa miezi ilopita tu eti saa hvi watu mtaani wameanza kuagiza Maji ya magari. Ni aibu.
Kama kuna tatizo kwenye miundombinu ya Maji waseme
 
Hatuna maji karibu mwezi mzima hapa hapa dsm salasala shida ni nini.
Tumekula eid el addha bila ya maji na umeme nao unaktwa hovyo hovyo tumechoka na hii hali. Tunahitaji majibu ya kina
 
Heri nyinyi mwezi, mtaani kwetu huku baada ya salamu ni yanatoka wapi? Umechota wapi? Kwa Mama nanii leo yanatoka.

Nakumbuka mara ya mwisho maji yalitoka january since hapo sijayaona wala kusikia habari zake😂Tanzaniaaa pyeee.
 
Mkuu umemuita Aweso aje ajibu suala la maji na umeme kwa pamoja? Anyways wanasema ukikosa maji kwa siku 3 mfululizo wasiliana na ofisi husika sijui umeshafika? Kama umefika hatua gani zilichukuliwa?
 
Back
Top Bottom