Kero ya foleni TAZARA: Je ni askari wa barabarani kushindwa kuongoza magari?

moudyjr

Senior Member
May 28, 2013
175
37
Tuchangie hoja bila matusi wala jazba nimeitoa sehemu:
[HASHTAG]#Foleni[/HASHTAG] kubwa ya magari TAZARA: Je ni askari wa barabarani kushindwa kuongoza magari ? Wananchi wahofia kupoteza 'vibarua'vyao.

=======

Ni takribani siku tatu sasa kumetokea foreni kubwaya magari kuliko wakati mwingine iliyowahi kutokea maeneo ya Tazara jiji la Dar es Ssalaam.Chaajabu ni kwamba foleni hiyo haikuweza kufahamika kisababishi chake ambapo baadhi ya raia wasafiri na watembea kwa miguu walionekana wakilalamika kuwa foleni hii haihusiani na ujenzi wa Fly Over Tazara kwani balabala zote mbili za daladala zinapitika hakuna kizuizi cha kusababisha foleni hiyo.

Kutokana na hali hiyo Quality Opportunity News iliamua kupanda moja ya daladala Gongo la Mboto kwenda Posta (nyerere road) na kuikuta foleni maeneo ya Ukonga (kutoka Tazara mpaka Ukonga) na kubaini ukweli huu hapa.

1.Hakukua na Ajari yoyote ile ambayo ingeweza aidha kusababisha foleni kubwa kiasi kile,
2.Ujenzi wa Fly Over haukuhusiani kabisa na Foleni kubwa kiasi kile
3.Makutano ya Jet Lumo,Airpot na banana havikuhusiana na ile foleni

Chaajabu baada ya kufika Tazara tulibaini kuwa foleni inatoka Tazara na kizuizi hakikuonekana kwani baada ya kuvuka mataa ya Tazara Kuelekea mjini (Nyerere Road) Kulikuwa kweupe kabisa lakini chaajabu tulikaa pale mataa ndani ya daladala dakika 40 ukiachana na huko nyuma tulikotoka.Baadhi ya abiria walionekana kukelwa na kitendo cha Traffic kupendelea gari za upande mmoja kwa mda mrefu sana na wengine kufikia hatua kusema traffic wanakula rushwa kwa watu wa maroli yanayotoka kurasini.

Kero wanazozipata wananchi

1.Baadhi ya abiria walisikika wakisema tutapoteza ajira zetu kwani nyumbani nimetoka saa 1 (moja) lakini mpaka sasa saa Nne kasorobo 9:45 na ofisini mda wa kazi ni saa mbili na nusu 8:30 Nitafukuzwa kazi ajira zenyewe ngumu hizi,maisha magumu.Alisikika abiria huyo.

2.Abiria mwingine ambaye anafanya kazi moja ya ofisi iliyopo Intava nyerere road alisema yeye alipewa barua ya warning (onyo) sasa hajui na leo amechelewa nini kitafuata.

3.Baadhi ya makondakta walidai kuwa traffic wanachukuwa rushwa kwa madereva wa maroli ili wawaite haraka, pia alidai wanaweka foreni makusudi ili wakamate magari yanayotanua na kuwalipisha faini.

Ndugu Kamanda Mpinga tunakuomba idara yako ichunguze swala hili la foreni Tazatra kwani bila kufanya hivyo maisha ya watanzania yatakuwa hatarini ikiwemo kupoteza ajira,vifo kwani wengine ni wagonjwa wanapelekwa hospitali na ukizingatia serikali hii ya Rais Magufuli iko kwaajiri ya kusaidia wanyonge kwani usafiri wa wanyonge ni daladala,mabosi hupanda private transport.
 
Vumilieni.... wa ubungo wanakumbuka ilivyokuwa enzi za kujenga dart
 
Me naona ujenzi wa flyover ndo umechangia kias kikubwa kwa foleni hiyo ila, baada ya ujenzi huo kukamilika sidhan kama kutakua na foleni kama kias hichi kwa sasa
 
Kila Siku hiyo barabara ina foleni lazima ukae 1hr kwenye foleni
 
kweli foleni ya tazara inatisha patupiwe jicho la ziada watu wanaumia

[QUOTE="MKWEPA KODI, post: 20985942, member:
 
Habari wana Jf...tangu saa6 nipo njian kutoka mbagala kwnd buguruni, na sasa hivi naandika uzi huu ndio kwanza nipo vetenary, ss huyu askari ina maana hatuon au sisi hatuna umuhimu??
 
Mwandishi wa makala hii alikuwa maeneo ya TAZARA kufanya Uchunguzi wa uhusiano wa ujenzi wa flyover na foleni amekuta havina uhusiano tuendelee kujadi sababu
 
Shida ya foleni Mandela Road haijaanza leo wala jana. Hili ni tatizo endelevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…