KERO: Mitandao ya simu ichunguzwe kwa kuwaunga wateja huduma bila ridhaa yao na kuwakata kwenye salio la kawaida

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
11,647
25,336
Moja kwa mmoja kwa hasira kubwa..

Ilikuwa haijawahi kunitokea zaidi ya kusikia kwa wenzangu kua mara nyingi unakuta mtu kaweka bocha ya ngama kufanyia shughuli mbalimbali unakuta ghalfa akijiunga salio halitoshi na akicheki salio wamekata kwa kweli inatia hasira sana. Na ukijaribu kuwapigia huduma kwa wateja wanakuambia umejiunga na huduma fulani ndio maana wamekata salio.

Leo nimeweka vocha halotel nijiunge kifurushi cha wiki kinachoisha ndani ya siku ghafla nimekuta wamekata Tsh 125/= kuwapigia wamesema kuna huduma nimejiunga labda wanisaidie kuiondoa ,mimi nikawaambia haina haja kwa vile leo ndio siku ya mwisho kuweka salio na ikiwezekana navunja line yao leo hii.

Binafsi sikuwahi kujiunga na huduma yeyote wala kupokea ujumbe kama umejiunga na huduma hii ,sasa maamuzi yangu sitoweka salio halotel mpaka mwaka upinduke na isingekuwa freebasic ningevunja na line yenyewe .

#UziTayari
 
Pole sana.

Imewahi kunipata vodacom na airtel.

Sikuwa nimejiunga kwa huduma yoyote.

Majibu ni hayo hayo.

Kuniondoa ilikuwa ngoma.

Naamini kuwa hili limo ndani ya uwezo wa TCRA iwapo watapenda kutuokoa.

Hata hivyo hili.nalo linaweza kuendelea kuwa hero kama ilivyo kero ya "Lips kwenye namba hii......."

TCRA tuokoeni na majanga haya.
 
Anayejua jinsi ya kukopa saloon halotel anielekeze nikope ili nihame vizuri nirudishe hasara yangu.
 
Nami ilishawahi notokea. Sasa kabla ya kuweka salio najiondoa kwanza kwenye huduma zao mbalmbali.
 
Kwa uzoefu kutokana na malalamiko ya watu mbalimbali mtaani Voda ndio kinara wa michezo hii japo kwangu hawajawahi kunifanyia michezo hiyo.
 
Pole sana.
Imewahi kunipata vodacom na airtel.
Sikuwa nimejiunga kwa huduma yoyote.
Majibu ni hayo hayo.

Kuniondoa ilikuwa ngoma.

Naamini kuwa hili limo ndani ya uwezo wa TCRA iwapo watapenda kutuokoa.
Hata hivyo hili.nalo linaweza kuendelea kuwa hero kama ilivyo kero ya "Lips kwenye namba hii......."

TCRA tuokoeni na majanga haya.
Waziri atakujana na jibu jepesi tu. "Watu wanajiunga na huduma za kufuatilia taarifa za vita ya urusi, hivyo linakatwa salio la kawaida kwasababu vita ni gharama."
 
Back
Top Bottom