Kenya yavunja Mikataba na Adani (Ruto aagiza taasisi husika kutafuta watoa huduma wengine kwa mchakato wa Upanuzi wa JKIA)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,461
22,837
Rais wa Kenya William Ruto, ameagiza kusitishwa kwa kandarasi ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKIA na ya nishati iliyopewa kampuni ya Adani kutoka India.

“Nilishawahi kusema huko nyuma, na narudia tena leo kwamba kutokana na ushahidi usio na shaka au taarifa za kuaminika kuhusu rushwa, sitositi kuchukua hatua madhubuti," Rais Ruto alisema.

" Naelekeza kwamba...wakala wa ununuzi ndani ya Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Uchukuzi. Nishati na Petroli zisitishe mara moja, mchakato unaoendelea wa shughuli ya upanuzi wa uwanja wa JKIA ambao ni ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, pamoja na mkataba wa usambazaji wa njia za umeme wa kampuni ya KETRACO uliohitimishwa hivi karibuni na mara moja kuanza mchakato wa kuhusisha washiriki wengine," aliagiza.

Mwezi Julai 2024 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini Kenya (KAA) ilithibitisha nia ya kampuni ya Adani kuhusishwa kwenye upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKIA, licha ya kampuni hiyo kutopewa kandarasi yoyote.

Hatua hiyo, ilichochea maandamano kutoka kwa wananchi, wakioneshwa kutokufurahishwa na maamuzi hayo, wakidai kuwa serikali ilikuwa inapanga njama za kuuza uwanja huo wa ndege wa kimataifa.

Haya yanajiri huku mamlaka moja nchini Marekani ikimshtaki mmiliki wa Kampuni ya Adani Holdings Limited ya India, bilionea Gautam Adani na watendaji wengine saba kwa tuhuma za rushwa na ulaghai wa dhamana kwa majukumu yao katika mpango wa mabilioni ya dola ili kupata fedha kutoka kwa wawekezaji wa Marekani na taasisi za kifedha duniani.

Washitakiwa hao ni pamoja na Adani, Sagar Adani na Vneet Jaain, watendaji wa kampuni ya India ya nishati mbadala ya Indian Energy Company.

Mkataba kati ya kampuni ya Adani na Kenya wa usambazaji ya umeme unagharimu zaidi ya dola milioni 700 ambao pia ulikuwa umeidhinishwa na Wizara ya Nishati ya Kenya.

Oktoba mwaka huu, kampuni ya Adani Energy Solutions ilitia saini mkataba wa miaka 30, wa dola milioni 736 wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi na Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Kenya. Mahakama nchini Kenya ilihairisha mkataba huo mwezi huo wa Oktoba.



My Take:
Kama wenzetu walishaanza kunyolewa wakakatisha katikati..., Je za kwetu tutie maji au ? Sababu haya mambo ya kuingia mikataba ya Ajabu na mwisho wa siku kuja kuivunja ndio maana kila leo tunalipishwa mapesa na walioingia mikataba hio hawawajibishwi (huenda ndio maana hizi tabia hazikomi); Chonde chonde walamba asali msiwe wasaliti kwa kuuza Taifa kwa ajili ya vijisenti ambavyo gharama yake ni mpaka wa vitukuu...

Soma pia

 
Pascal Mayalla ; Huu ndio Uzalendo kama mdau tu anakuwa whistle blower nyie magwiji wa Habari mnatuletea nini zaidi ya Udaku


View: https://youtu.be/BAc48miwjeA?si=D5LZHE3Q4KSC1M3D
Mkuu Logikos , uzalendo, huo, hata sisi tunao, ila kitu muhimu cha kwanza ni usalama kwanza. Jamaa yuko Paris ndio maana kaweza, hili jambo kuhusu waandishi wa habari wa Tanzania nimewahi kulisema humu. Thread 'Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...' Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Niko kwenye process ya kuirelocate PPR US, nikifanikiwa nahamia US, then, nami nitaanza kushuka na nondo kama hizi.
P
 
Hongera sana utakuwa umeitendea haki tasnia yako ila unajua hata huko kama ukiguza maslahi yao hawachelewi kusema hayo ni mambo ya national security (mfano Snowden) au hata kuziba uchunguzi mfano Tony Blair na BAE

Au kupigwa jungu kwamba umenunuliwa na Mabeberu mfano yule mwandishi UK; Ila unaweza ukawa kama Mange ila badala ya UDAKU wa maisha ya watu ukaleta mambo ya Raslimali za Taifa...

Ndio maana hapa nilishawahi kusema tuwe na total transparency iwapo kuna mambo yanahusu mali za UMMA....kuwe na TOTAL TRANSPARENCY...

Na kama sio hivyo atleast itungwe Sheria ya Waandishi kuweza kuangalia chochote na kuuliza lolote kuhusu mali ya UMMA na watumishi wa UMMA (hata wanasiasa tunaowalipa Ruzuku) na walazimishwe kujibu lolote wakati wowote

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…