Kenya yafanikiwa kurusha Satelite yake kwenye mzingo wa Dunia kwa kutumia Roketi, Tanzania kufanya hivyo mwaka 2025

GP Logistics Company

JF-Expert Member
Feb 12, 2022
407
548
Nchi ya Kenya wamefanikiwa kurusha satellite yao kwenda anga za mbali muda mchache uliopita ikiwa imesafirishwa ndani ya rocket ya Falcon 9 kutokea huko katika kambi ya Vendeberg space center

Mara baada ya majaribio matatu kushindikana siku chache za nyuma kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo huwa ni hatari sana kwa vyombo vinavyosafiri anga za mbali

Mpaka muda huu kila satellite iliyobebwa ndani ya rocket ya Falcon 9 zimeshabaki zenyewe zikiendelea na safari za kuelekea katika eneo lake rasmi , kumbuka rocket hiyo ilibeba jumla ya satellite 50 za kutoka katika taasisi binafsi na zile za serikali

Mara baada ya satellite ya Taifa 1 kufika katika eneo lake lengwa basi Nchi ya Kenya rasmi itakuwa na satellite anga za mbali inayofanya kazi kubwa ya kwenye kilimo na mambo mbalimbali ya ulinzi

Kampuni binafsi ya DIGXAM yenye asili ya Kitanzania inayomiliki mtandao wa onlibe business www.digxam.co inatarajia kurusha satellite yake baada ya kukamilika 2025 kwajili ya matumizi yake binasi ya kitekinolojia na biashara kwa kushirikia na Wajapan.

Hii itakuwa kampuni ya kwanza binafsi kumiliki satellite yake Africa na baadhi ya mabara mengi pia itapandisha heshima nchi yetu ndani na nje ya Africa.
 
Kenya jafanikisha jaribio la kwanza la kurusha satellite nje ya Dunia
Je una mawazo gani kuhusiana na jambo hili ? Na sisi nchi za Africa mashariki kwa nini tusifanikishe swala kama hili
Tukumbuke Kenya wana mpango wa kuanzisha Coding subject kwa wanafunzi kuanzia primary schools
 
Kenya imepeleka Satelaiti yake ya kwanza katika mzingo wa dunia, kwa kutumia roketi lililofyatuliwa kutoka California, Marekani, ripoti ya Shirika la anga za mbali la Nchini Marekani la SpaceX zimethibitisha.

@dw_kiswahili inaripoti kuwa kurushwa kwa Satelaiti hiyo kulitarajiwa majira ya usiku muda wa Marekani Jumatatu wiki hii lakini kulicheleweshwa mara kadhaa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Satelaiti hiyo ya Kenya ilisanifiwa na kikundi cha Watafiti kutoka Kenya na inanuia kutoa data za kilimo na kuchunguza mabadiliko ya kimazingira nchini Kenya, hususan wakati huu nchi hiyo inapokabiliwa na ukame wa muda mrefu.

Pattern Odhiambo, Mhandisi wa Shirika la Kenya la Anga za Mbali, KSA, amesema satelaiti hiyo iliyopewa jina la Taifa 1, itakuwa na faida za moja kwa moja katika sekta za utafiti na kuboresha mavuno ya kilimo.

Hadi mwaka 2022, Satelaiti zipatazo 50 za Mataifa ya Afrika zilikuwa zimepelekwa kwenye mzingo wa dunia, kulingana na Shirika la Nigeria linalofuatilia mipango ya Afrika ya anga za mbali.
 
Ni swala la priority Kenya wanapenda sana kujimwambafai wakati raia wao kule Turkana wanakufa najaa, kibela slum ndo kubwa barani Africa wana high urban poverty rate, hizo pesa za stilate wange anza na kujengea raia wao simple and cheap residential houses, nakununulia watu wao chakula wasife njaa.
Tanzania imewajengea nyumba wananchi wa wapi?
 
Ni swala la priority Kenya wanapenda sana kujimwambafai wakati raia wao kule Turkana wanakufa najaa, kibela slum ndo kubwa barani Africa wana high urban poverty rate, hizo pesa za stilate wange anza na kujengea raia wao simple and cheap residential houses, nakununulia watu wao chakula wasife njaa.
Umeongea jambo jema sana, kwa Kenya raia wana hali mbaya
 
Kwa Tanzania, kama itarushwa na kampuni binafsi, hiyo itafanya kazi iliyokusudiwa.

Lakini kama itarushwa na Serikali, uwezekano mkubwa hakutakuwa na msaada wowote zaidi ya upotevu wa pesa. Kama Serikali inashindwa hata kusimamia huduma tu ya umeme ambayo tekinolojia ya chini kabisa, umeme ambao vyanzo vyake unaviona kila siku, nyaya na nguzo unaziona kila siku, itakuwa hivyo ambavyo vikirushwa havitakuwa vikionekana jwa macho yetu!!
Sio kwajili ya kazi za Kitaifa ka ya Kenya ni kwajiki ya kazi zake binafsi nfano server hosting space internet nambo kama hizo nfano kampuni inayomiliki mtandao wa Facebook whatspp pia wana satellite kwenye orbit kwajili ya uendeshaji wa mitandao yao bila kutumia server za kukodi au za makampuni mengine.
 
Kenya jafanikisha jaribio la kwanza la kurusha satellite nje ya Dunia
Je una mawazo gani kuhusiana na jambo hili ? Na sisi nchi za Africa mashariki kwa nini tusifanikishe swala kama hili
Tukumbuke Kenya wana mpango wa kuanzisha Coding subject kwa wanafunzi kuanzia primary school

hii ni dunia ya kidigital firebase wanatafuta watu wenye kujua code duniania kote ajira nje nje Kenya wameona mbali sana
 
Kama wewe ni STD 4 B uwezi kuelewa kitu kuhusu satellite nenda shule.
Idiot...sio wote walioenda shule wanajua kila jambo. Ungekuwa muungwana ungeweza kutoa elimu kunijulisha kuliko ulivyojibu. Bora mimi niliyeomba msaada wa kujulishwa kuliko wewe muungwana ambaye hauna hekima wala busara.
 
Idiot...sio wote walioenda shule wanajua kila jambo. Ungekuwa muungwana ungeweza kutoa elimu kunijulisha kuliko ulivyojibu. Bora mimi niliyeomba msaada wa kujulishwa kuliko wewe muungwana ambaye hauna hekima wala busara.
Mkuu mbona unani mind mim sijarusha satellite 🛰 sijajosema satrellite wala siwezi kufundisha mtu chochote kuhusu 🛰 📡 pia mim sio mkenya Kawaukize wakenya hii nitarifa tu
 
Back
Top Bottom