Kenya warusha satellite angani

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,468
Nchi ya Kenya wamefanikiwa kurusha satellite yao kwenda anga za mbali muda mchache uliopita ikiwa imesafirishwa ndani ya rocket ya Falcon 9 kutokea huko katika kambi ya Vendeberg space center

Mara baada ya majaribio matatu kishindikana siku chache za nyuma kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo huwa ni hatari sana kwa vyombo vinavyosafiri anga za mbali

Mpaka muda huu kila satellite iliyobebwa ndani ya rocket ya Falcon 9 zimeshabaki zenyewe zikiendelea na safari za kuelekea katika eneo lake rasmi , kumbuka rocket hiyo ilibeba jumla ya satellite 50 za kutoka katika taasisi binafsi na zile za serikali

Mara baada ya satellite ya Taifa 1 kufika katika eneo lake lengwa basi Nchi ya Kenya rasmi itakuwa na satellite anga za mbali inayofanya kazi kubwa ya kwenye kilimo na mambo mbalimbali ya ulinzi

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1681555883593.jpg
 
Ni mambo ya fedha tu, ata na Sisi tukiamua tunalipa na wanaturushia ya kwetu angani
 
Wakuu, nimeona habari Al Jazeera kwamba Kenya wamefanikiwa kurusha satellite yao angani. Je, Tanzania tunakwama wapi? au uwezo wetu katika nyanja za sayansi na teknolojia umeishia kwenye mbio za mwenge.
Karibuni.

===​
Kufikia 2022, angalau nchi 13 za Afrika zilikuwa zimetengeneza satelaiti 48, lakini hakuna iliyorushwa kutoka ardhi ya Afrika.

Kenya itarusha setilaiti yake ya kwanza inayofanya kazi wiki ijayo katika mafanikio makubwa ya mpango wa anga za juu nchini humo, serikali ilisema Jumatatu.

Taifa-1, au taifa moja la Kiswahili, imeratibiwa kurushwa Aprili 10 kwa kutumia roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka Vandenberg Space Force Base huko California.

"Misheni hiyo ni hatua muhimu," wizara ya ulinzi na Shirika la Anga za Juu la Kenya zilisema katika taarifa ya pamoja, na kuongeza kuwa itachangia kwa kiasi kikubwa "uchumi wa anga za juu unaochipuka" wa nchi.

Satelaiti hiyo ya uchunguzi "imeundwa na kuendelezwa kikamilifu" na wahandisi wa Kenya na itatumika kutoa data kuhusu kilimo na usalama wa chakula, miongoni mwa maeneo mengine, ilisema taarifa hiyo.

Upimaji na utengenezaji wa sehemu ulifanyika kwa ushirikiano na mtengenezaji wa anga wa Kibulgaria, iliongeza.

Kenya, taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi katika Afrika Mashariki, inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa baada ya misimu mitano ya mvua kushindwa.

Urushaji wa satelaiti utaongeza msukumo kwa mataifa ya Afrika kwa uvumbuzi wa kisayansi na maendeleo ya programu za anga.

Misri ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutuma satelaiti angani mwaka 1998.

Mnamo 2018, Kenya ilizindua nanosatellite yake ya kwanza ya majaribio kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

Kufikia 2022, angalau nchi 13 za Kiafrika zilikuwa zimetengeneza satelaiti 48, kulingana na Space in Africa, kampuni yenye makao yake makuu nchini Nigeria inayofuatilia programu za anga za juu za Afrika. Ni pamoja na Ethiopia, Angola, Afrika Kusini, Sudan na nyinginezo.

Zaidi ya satelaiti 50 za Kiafrika zimerushwa kufikia Novemba 2022, kulingana na Space in Africa, ingawa hakuna hata moja kutoka ardhi ya Afrika.

Mnamo Januari, serikali ya Djibouti ilitangaza mkataba wa maelewano na kampuni ya Hong Kong kujenga kituo cha anga cha kibiashara cha $1bn ambacho kinatarajiwa kuchukua miaka mitano kukamilika.
 
Either viongozi wanauwelewa mdogo au ni wabinafsi wasio na nia ya dhati kuiendeleza nchi.

Kwa mfano, nilikua na project yangu, nikaweza home server, nilifeli, umeme mvua ikianza tu unakata, sikuweza kua na ups kubwa.

Wangeanza kuimarisha nishati wakaacha siasa, kisha wakachagua wataalamu kwa uwezo wao na sio mtoto wa baba mdogo.

Wanasayansi wengi huwa wanaandaliwa na wanachujwa tangu wakiwa wadogo. It is not an overnight process.
 
Wakuu, nimeona habari Al Jazeera kwamba Kenya wamefanikiwa kurusha satellite yao angani. Je, Tanzania tunakwama wapi? au uwezo wetu katika nyanja za sayansi na teknolojia umeishia kwenye mbio za mwenge.
Karibuni.​
Ripoti ya CAG ni satelite tosha.

Na hairukki leo wala.kesho

Watu wapo bize kusaka madaraka na chawa wapo bize kubeba mabegi ya wasaka vyeo
 
Kila la kheri majirani...

Unga juu, mishahara mnashindwa kulipana kumbe pesa mnapeleka angani...
 
Back
Top Bottom