Kenya, Tanzania, na Uganda zitwaeni Burundi, DRC, na Rwanda ili kuleta amani na maendeleo

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
7,523
8,862
1738256704382.png

Tokana na chokochoko, migongano, migogoro, vita, na wizi nchini DRC, nashauri mataifa tajwa hapo juu yatie buti kwenye nchi hizo na kuzitwaa ili kuunda taifa moja kubwa na tajiri haraka. Tukizitwaa, DRC itasaidia kutoa ardhi kwa viinchi visivyo na ardhi ya kutosha kama Burundi, Rwanda, na Uganda.

Pia, tutatokomeza ukabila na migongano isiyo na tija kwa eneo letu. Mbali na hiyo, taifa jipya litakaloundwa, mbali na kuwa na nguvu na raslimali, litatoa mwongozo na mwelekeo juu ya kuunganisha bara la Afrika.

Mali tunazo lakini tunazikalia huku watawala wetu wakisifika kwa kulalamika na kuombaomba wakati raslimali zipo bwerere. Japo hii ni hypothesis, ikifanyiwa kazi, tunaweza kujikomboa, kuwakomboa wahanga na Afrika kwa ujumla. Wabaya wetu wanaungana. Sisi tunagawanyika, kuchukiana na kuhujumiana. Tutangaze vita ya ukombozi wa kuunganisha bara letu.

Kuna faida nyingi kwenye wazo hili kama ifuatavyo:
Mosi, tutakomesha ukabila, ujambazi wa kimataifa na ununuzi wa silaha visivyo na tija,
Pili, tutatoa mwelekeo kwa bara la Afrika na kuonyesha faida za kuungana,
Tatu, tutazuia genocides zinazongoja kutokea.
Nne, tutaleta amani, maendeleo na usalama kwao na kwetu,
Tano, tutatoa dozi ya chokochoko zisizo na kichwa wala miguu,
Sita, tutaunda na kujenga taifa kubwa, lenye nguvu na utajiri.
Nawaza tu. Sijui wanabodi mnaonaje na kusemaje?
 

View attachment 3218936

Tokana na chokochoko, migongano, migogoro, vita, na wizi nchini DRC, nashauri mataifa tajwa hapo juu yatie buti kwenye nchi hizo na kuzitwaa ili kuunda taifa moja kubwa na tajiri haraka. Tukizitwaa, DRC itasaidia kutoa ardhi kwa viinchi visivyo na ardhi ya kutosha kama Burundi, Rwanda, na Uganda. Pia, tutatokomeza ukabila na migongano isiyo na tija kwa eneo letu. Mbali na hiyo, taifa jipya litakaloundwa, mbali na kuwa na nguvu na raslimali, litatoa mwongozo na mwelekeo juu ya kuunganisha bara la Afrika. Mali tunazo lakini tunazikalia huku watawala wetu wakisifika kwa kulalamika na kuombaomba wakati raslimali zipo bwerere. Japo hii ni hypothesis, ikifanyiwa kazi, tunaweza kujikomboa, kuwakomboa wahanga na Afrika kwa ujumla. Wabaya wetu wanaungana. Sisi tunagawanyika, kuchukiana na kuhujumiana. Tutangaze vita ya ukombozi wa kuunganisha bara letu.​

Kuna faida nyingi kwenye wazo hili kama ifuatavyo:​

Mosi, tutakomesha ukabila, ujambazi wa kimataifa na ununuzi wa silaha visivyo na tija,​

Pili, tutatoa mwelekeo kwa bara la Afrika na kuonyesha faida za kuungana,​

Tatu, tutazuia genocides zinazongoja kutokea.​

Nne, tutaleta amani, maendeleo na usalama kwao na kwetu,​

Tano, tutatoa dozi ya chokochoko zisizo na kichwa wala miguu,​

Sita, tutaunda na kujenga taifa kubwa, lenye nguvu na utajiri.​

Nawaza tu. Sijui wanabodi mnaonaje na kusemaje?​

Hujui unachokiongea
 
Back
Top Bottom