Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,569
- 4,228
KenGold imemsajili winga wa zamani wa Yanga na Simba, Bernard Morrison kwa mkataba wa miezi sita huku ikikaribia kuwanasa Kelvn Yondani na Obrey Chirwa.
Timu hiyo inaonekana kuweka kipaumbele kwa wachezaji huru ili kutolipa ada za uhamisho katika dirisha hili dogo la usajili linaloendelea kwa vile watatu hao wote hawana mikataba na timu nyingine.
Uhakika wa kusajiliwa Morrison ulianza kuthibitika jana baada ya kuona picha akiwa amepokewa na mtendaji mkuu wa KenGold, Kenneth Mwambungu mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya.
Taarifa za uhakika ambazo Mwananchi Digital inazo ni kwamba tayari Morrison ameshasaini mkataba wa miezi sita na muda mfupi ujao atatambulishwa rasmi.
KenGold pia inaripotiwa imeshafikia makubaliano na Kelvin Yondani na Obrey Chirwa ambao tayari wapo jijini Mbeya kukamilisha usajili huo.