Kelele za Rais Magufuli bila hawa watanzania ni debe tupu!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991

These are the six most powerful people in Tanzania!

Kwa nchi kama Tanzania ambayo ina taasisi zisizo imara, Hawa ndiyo macho, masikio na maisha ya Rais magufuli.

Ni kweli madaraka ni dhamana lakini kwa nchi kama Tanzania, madaraka ya juu ni zaidi ya dhamana.

Kelele anazopiga Rais Magufuli kuhusu kubomoa watu ambao watamkwamisha katika kazi zake yatakuwa hayana maana yoyote kama yatakuwa hayajapata baraka kutoka kwa hawa Watanzania ambao wako sita.

Hiki ni kikundi cha watu wanaoifahamu vizuri Tanzania na kuna wengine kati yao hata ukichukua picha yake na kuanza kuwahoji Watanzania kama wanawafahamu, ninaamini ni watanzania wachache wanawafahamu.

Mmojawapo kati yao anaweza kuibadilisha Tanzania kutoka utawala wa kiraia mpaka utawala wa kijeshi. MwL. Nyerere anafahamu vizuri kutokana tukio lililotokea Tarehe 20 Januari 1964.

Mmojawapo kati yao anaweza kufanya maisha ya raia au kisiasa kwa wanasiasa kuwa niya wasiwasi nchini. Viulize vyama vya siasa kwa kinachotokea kwa sasa.

Mmojawapo ana uwezo wa kufahamu hali halisi ya kiusalama nchini na pia ana uwezo wa kumzuia au kumruhusu Rais Magufuli kwenda sehemu yoyote na wakati wowote iwe nchini au nje ya nchi. Muulize Mzee Peter Bwimbo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi wa viongozi, (Presidential Securty Unit) wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere.

Mmojawapo anaweza kufanya maisha yako gerezani kuwa mazuri au mabaya. Muulize aliyekuwa Waziri wa fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Mmojawapo kati yao anaweza kuzifanya kazi zako au biashara zako kuwa katika wakati mgumu kama akiamua kukufuatilia kwa karibu. Muulize Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola, Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa na Mbunge wa jimbo la Mvomero Sadick Murad.

Mmojawapo anaweza kukuruhusu kuwa Mtanzani au la. Muulize Jenerali Ulimwengu.

Kinadharia (theoretical) unaweza kutokubaliana na angalizo langu lakini kiuhalisia (practical) huwezi kupambana na ukweli wa angalizo langu.
 
Ww mtazamo wako ni mdogo sana, hao ni watanzania wenzetu tuliowapa mamlaka kupitia rais ambae anachaguliwa kwa kura za watu wote, so iman inaanza kwa rais then yy ana delegate hiyo iman kwa hao wakuu. Ni kwa sababu ccm imeharibu hii nchi lakin hakuna sababu kabisa ya kuwachukia hao wajamaa kwa sababu mambo ambayo wapinzani wanapigania yanamgusa kila mtu wakiwemo hao, mfano ukiacha IGP na CDF foleni inatukumba wote, umeme unakatika kote vyote hiv ni outcome ya sera mbovu za ccm.

Nikija kweny point yako, nchi inaendeshwa kwa kodi, na sio kitu kingine chochote, kama unafurahi unapoona watu wanapigwa basi uwezo wako ni mdogo sana, siku wapinzani wakawashawishi watu waache kulipa kodi, na waanze kuficha hela zao ndani, ndo utaujua umuhimu wa kula vizuri na kipofu.
 
Tafsiri mojawapo iliyo wazi ktk andiko lako ni kwamba hawa watu wana nguvu kubwa ya kuweza kutumia mamlaka yao vibaya au hata kinyume cha sheria.
 
Natetemeka mikono na kajasho kembamba kananitoka nikiziona hizo sura kwani naziogopa ajabu! Usiombe wakugeuke japo utawachukulia poa kabla. Kama hukwenda jkt miaka ya 80s huwezi kujua lolote juu ya hao watu. Wakisema wote mlale SAA 12 jioni wanamaanisha. Naogopa kuwajadili kwani Nina force number.
 
Tafsiri mojawapo iliyo wazi ktk andiko lako ni kwamba hawa watu wana nguvu kubwa ya kuweza kutumia mamlaka yao vibaya au hata kinyume cha sheria.
Hoja yako kimantiki nimeijibu katika sentensi hii;
''Kwa nchi kama Tanzania ambayo ina taasisi zisizo imara, Hawa ndiyo macho, masikio na maisha ya Rais magufuli''.
 
Nitofautiane na wewe kwenye hili. Unafikiri hao wanaweza ku command chochote kinyume na sheria na wengine wakatii? Mfumo wa usalama wa Tanzania haumpi nafasi yeyote kuamua lolote bila kupata vikwazo vizito kama vipo kinyume na sheria. Hivi unaanzaje kushawishi majenerali wote wa jeshi kutii amri yako iliyo kinyume kikatiba na sheria za kijeshi? Hao ni powerful kwenye command za kikatiba na si vinginevyo.
 
Kumbuka amri inatoka wapi
 
Kwanza nadhani hujaelewa mantiki ya thread yangu.

Pili, Mimi ninaongelea mazingira ya utawala waTanzania, wewe unaongelea theories za utawala na sheria huku ukichanganya na itikadi za vyama.

Jaribu kusoma vizuri ili uelewa vizuri mantiki ya thread yangu.
 
Na SAUTI ya mwisho na maamuzi ya UHAKIKA ni sisi WANANCHI tukiamua kabisaa kabisaa.Muulize David Cameron.
Tanzania ni ya watanzania na si kikundi cha watu.SOMO HILO ELEWA
 
Duh na Makonda pia?

Mbona hao wote kama ni wale kwenye list ya kuwateua yeye?
 
Hawo watu sita alowataja ni makada wa CCM na alowapa cheo ni Raisi
kwa hivyo kulinda nyadhifa zao watafanya kazi kutumikia CCM na kumtumikia Raisi.

Hakuna Demokrasia Tanzania

Umesahau Mwana sharia mkuu pia ni CCM na muengeze kwenye list.
 

These are the six most powerful people in Tanzania!

Kwa nchi kama Tanzania ambayo ina taasisi zisizo imara, Hawa ndiyo macho, masikio na maisha ya Rais magufuli.

...
Hao sita na zingine 16 ndio zinasaidia chama cha majipu na ufisadi kubaka demokrasia Tanzania, kuirudisha nyuma demokrasi na kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya DOMOkrasi.

Over 33 million people from England, Scotland, Wales, Northern Ireland and Gibraltar have all had their say.

We should be proud of the fact that in these islands we trust the people for these big decisions.

We not only have a parliamentary democracy, but on questions about the arrangements for how we've governed there are times when it is right to ask the people themselves and that is what we have done. "There can be no doubt about the result"

The British people have voted to leave the European Union and their will must be respected.

LINK David Cameron announces his resignation - full statement

Hapa Tz anatokea Kivuitu na nambari zake za kupanga na kupangua anakutangazia mtawala anayemtaka yeye au anafuta uchaguzi na kufanya igizo jengine la uchaguzi la kuleta ushindi wa kishindo na kwa kishindo.
 
Hakuna kitu hapo. Lubuva ndio kila kitu. Kama ilivyo Jecha kwa Zenji
 
Ndio maana nchi inaliwa.
Jinsi ulivyowaongelea ni kwamba wenyewe hawana uchafu
Na tuwaogope kama Miungu. Usitutishe maisha bana.
Wapoteze vitambi kwanza, hivyo vitambi ni ugonjwa.
 
Ukipita katika anga zao lazima utatetemeka!

Umenikumbusha maisha ya JKT siku ambayo ilikuwa ni siku yangu ya kwanza kurepoti.

Nilizamia Makutupora lakini sikufanikiwa kubaki hapo badala yake tukapewa transfer ya kwenda Bulombora ambako ndiko nilikuwa nimepangiwa.

Siku ambayo tulifika Makutupora getini nilipatwa na mshangao kuona watu kama wanakimbia hovyo na hakuna aliyekuwa anatembea.

Tulikutana na afande akatuambia tuchuchumae na kuanza kuruka kichura kwa sababu tulikuwa tunatembea wakati haturuhusiwi kutembea.

Umenikumbusha mbali sana!
 
Umemsahau Mtu mmoja anayeitwa "Mtanzania" a.k.a Mwananchi, ambaye akiamua kulianzisha, hata maisha ya hao uliowataja nayo yatakuwa hatarini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…